Nafasi Ya Matangazo

August 04, 2018

Kamisha Jenerali wa Jeshi la Magereza  nchini Phaustene Kasike akisalimiana na maofisa wa ngazi ya juu katika jeshi hilo mkoa wa Kilimanjaro.
Kamishana Jenerali wa Magereza,Phaustine Kasike pamoja na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Onesmo Buswelu (mwenye suti katikati) wakipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kiwanda cha Viatu-Karanga,Ezron Nganoga.
Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Karanga Leather Industries Co,Ltd Masoud Omar akitoa maelezo kuhusu mitambo mipya iliyofungwa katika kiwanda hicho kwa Kamishana Jenerali wa Magereza .
Kamisha Jenerali wa Magereza akitizama bidhaa za viatu ambazo zilinazalishwa katika kiwanda cha Viatu cha Karanga kinachomilikiwa kwa ubia kati ya uliokuwa mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PPF) na Jeshi la Magereza.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza ,akitazama bidhaa mbalimbali za Viatu zinazozalishwa na kiwanda hicho.
Baadhi ya Askari Magereza wakifanya kazi za uandaaji wa Bidhaa za Viatu katika kiwanda hicho.

Sehemu ya Mitambo mipya iliyofungwa katika Kiwanda cha kutengeza Viatu cha Karanga Moshi.
Sehemu ya Bidhaa za viatu vinavyozalishwa katika kiwanda hicho.
Kamishna Jenerali wa Magereza ,Phaustine Kasike akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wengine wa jeshi hilo pamoja na wageni mbalimbali.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.


Na Dixon Busagaga,Moshi.
MRADI wa Kiwanda cha kutengeneza Viatu cha Karanga Leather Industries Co.Ltd upo katika hatua ya mwisho kukamilika baada ya kufanyika maboresho katika ufungaji wa mitambo mipya ya kukata na kushona ngozi pamoja na mfumo wa umeme katika kiwanda hicho.

Kampuni inayosimamia Kiwanda cha kutengeneza Viatu cha Karanga -Moshi, ilianzishwa Mei 30 mwaka jana kwa ubia kati ya uliokuwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii PPF na Jeshi la Magereza ,ambapo awali kilikuwa kikizalisha jozi 150 kwa siku.

Baada ya Maboresho kukamilika kiwanda hicho sasa kitaweza kuzalisha Jozi 400 kwa siku na kutokana na sasa kuweza kuweka soli za viatu,kushona ngozi na kazi nyingine.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini ,Phaustine Kasike pamoja na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Onesmo Buswelu wametembelea Kiwanda hicho kujionea maboresho hayo ambayo yanakadiliwa kufikia kiasi cha Sh Bil 2.7 katika uwekezaji wa Mitambo na kuoneshwa kuridhishwa.
Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kutembelea Kiwanda hicho,kamishna Jenerali Kasike amesema ujenzi wa miradi hiyo miwili pamoja na utekelezaji wa agizo la Rais kuwa na Tanzania ya  Viwanda ,lakini pia itaongeza ajira na kuwawezesha wafungwa kuwa na ujuzi ambao watautumia kuajiri na kujiajiri baada ya kutukimikia kifngo.

Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Onesmo Buswelu amesema mradi huo pia utaongeza thamani ya Mifugo kwa afugaji wa Ng’ombe ,Mbuzi na Kondo kwa kuwa pembe kwato na ngozi za kifugo hiyo itatumika kama malighafi katika viwanda hivyo.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Kampuni inayosimamia Kiwanda cha Viatu –Karanga ,Masoud Omary amesema awamu ya pili ya mradi huo imeanza kwa uchoraji wa ramani ya majengo ya kiwanda pamoja na ununuzi wa mitambo huku Mkurugenzi wa Uhandisi na Maendeleo ya Viwanda Mhandisi ,Lugano Wilson akieleza namna ambavyo kiwanda kitakuwa.

Awamu ya pili ya mradi huo utakaohusisha ujenzi wa kiwanda kikubwa cha Kisasa kwa nchi za Afrika Mashariki na kati unataji kugharimu kiasi cha Sh Bil 67 kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha jozi 4000 kwa siku huku watanzania zaidi ya 3000 wakipata ajira.

Baada ya Mifuko ya Hifadhi za Jamii kuunganishwa ,sasa uwekezaji huo uliokuwa chini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PPF) utaendelea chini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa umma (PSSSF) ambapo utafanyika ujenzi wa kiwanda cha Viatu,ujenzi wa kiwanda cha kuchakata Ngozi,utengenezaji wa soli za viatu pamoja na kiwanda cha bidhaa mbalimbali za Ngozi.
Posted by MROKI On Saturday, August 04, 2018 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo