Balozi Dkt. James Alex Msekela akikabidhi uenyekiti wa Kundi la G77 na China Umoja wa Mataifa Geneva kwa Balozi. Farukh Amil wa Pakistani Januari 17, 2017.
Balozi wa Tanzania Ofisi za Umoja wa Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, Geneva, UswisiDkt. James Alex Msekela, akiongoza mkutano wa kukabidhi Uenyekiti wa Kundi la G77 na China Januari 17, 2018 baada ya kuongoza kundi hilo kwa mafanikio makubwa mwaka 2017 ambapo Tanzania ilikuwa Mwenyekiti.
Balozi Dkt. James Alex Msekela akiwa katika picha ya pamoja na Dkt. Mukhisa Kituyi (katikati), Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo (UNCTAD) na Balozi Amil wa Pakistani wakati wa hafla ya makabidhiano ya uenyekiti wa Kundi la G77 na China, Geneva Uswisi. UNCTAD na kundi la G77 na China zinauhusiano wa kihistoria kutokana na kuwa Shirika hilo lilianzishwa kwa msukumo wa nchi za kundi hilo katika Umoja wa Mataifa kwa lengo la kushughulikia vikwazo vya Biashara, uchumi na maendeleo vinavyokabili nchi zinazoendelea.
0 comments:
Post a Comment