SIKU chahche baada ya Sekretarieti ya Shirikisho la Soka Nchini TFF kutoa taarifa ya kuwafikisha katika Kamati ya maadili viongozi wanne wa Soka kwa thuya za kughushi na udanganyifu, Uongozi wa Soka mkoa wa Mtwara kupitia Mwenyekiti wake Athman Kambi umezungumza.
Mwenyekiti wa Chamacha Soka Mkoa wa Mtwara (MTWAREFA) Athman Kambi amesema Chama Chake Kinatambua FORM Inayoonesha mapato ya shilingi Million 37.7 yaliyopatikana katika Mchezo wa Ndanda FC dhidi ya Simba FC uliochezwa Desemba 30 katika uwanja wa Umoja Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara.
Viongozi wanaotuhumiwa ni pamoja na msimamizi wa Kituo cha Mtwara Dunstan Mkundi, Katibu wa Chama cha soka mkoa wa Mtwara Kizito Mbano, Muhasibu msaidizi waklabu ya Simba Suleiman Kahumbu na Katibu msaidizi wa Klabu ya Ndanda FC ya Mtwara Selemani Kachele. wa Tuhuma za Kughushi Nyaraka,Chama Cha Soka mkoa wa Mtwara Kimeibuka na Kutoa Tamko.
Aidha kambi amekiri kuwa licha ya kuwa bado haijathibitishwa lakini Tuhuma Hizo zimeonesha Taswira Mbaya katika soko la Mkoa wa Mtwara
Kwa mujibu ya kanuni za Shirikisho ya Chama cha Mpira wa Miguu Nchini (TFF) mapato yanayopatikana baada ya Mechi Asilimia 40 yanakwenda kwa timu mwenyeji,asilimia20 kwa timu inayocheza Ugenini,uwanja asilimia 15 na TFF wanapata asilimia5.
0 comments:
Post a Comment