Nafasi Ya Matangazo

January 13, 2018

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam,  Ali Hapi, (katikati), akiteremka kutoka juu ya tenki kubwa la kuhifadhia maji linalojengwa huko Mabwepande nje kidogo ya jiji, wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya maji wilayani kwake Januari 13, 2018.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MKUU wa wilaya ya Kinondoni Ali Hapi, amewataka wakandarasi wanaotekeleza ujenzi wa mradi wa uboreshaji wa huduma za ugawaji na usambazaji maji wilayani kwake kuongeza kasi ya kukamilisha mradi huo kama ambavyo mkataba unaelekeza.

Hapi aliyasema hayo leo Januari 13, 2018 mwishoni mwa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundomnbinu hiyo inayohusisha matenki makubwa manne na vituo vinne vya kusukuma maji (Booster Stations) ikiwa ni pamoja na utandikaji  wa mabomba ya kusafirisha maji.

Mradi huo ambao unatekelezwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka jijini Dar es Salaam, (DAWASA), ni sehemu ya mradi mkubwa wa uboreshaji wa huduma za ugawaji na usambazaji maji katika baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Pwani,  Dar es Salaam, sehemu ya mikoa ya Morogoro na Tanga na ulianza kutekelezwa mwezi Machi 2016. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

“Mradi huu ulipaswa kuwa umekamilika Novemba mwaka jana, lakini hatua waliyofikia baadhi ya maeneo wako asilimia 80, mengine asilimia 75 na mengine asilimia 50, ahadi yao ni kwamba ndani ya kipindi kifupi kijacho wataweza kukamilisha mradi huu.” Alisema

Hata hivyo Hapi amepongeza usimamizi na ufuatiliaji wa karibu unaofanywa na mamlaka husika zinzosim amia mradi huo. “Niwapongeze DAWASA na DAWASCO kwa kazi nzuri ya kuhakikisha wanasimamia na kufuatilia utekelezaji wa mradi huu.” Alisema Hapi.

Alitaja maeneo yatakayofaidika na mradi huu kuwa ni pamoja na wakazi wa Makongo, Changanyikeni, Salasala, Bunju, Mabwepande na Wazo.

“Mradi ukikamilika utaondoa kero ya maji katika wilaya yetu  kwa asilimia 95, kwa hivyo, hii nifaraja kubwa kwa wananchi wa Kinondonbi hususan katika maeneo nilkiyoyataja.” Alifafanua.
 Hapi, akimsikiliza Mkandarasi,   Mhandisi P.G. Rajani wa kampuni ya WAPCOS limited ya India, alipotembelea sehemu ya ujenzi wa mtambo wa kusukuma maji huko Salasala jijini Dar es Salaam.
Hapi, akimsikiliza Mkandarasi,   Mhandisi P.G. Rajani(kulia) wa kampuni ya WAPCOS limited ya India, alipotembelea sehemu ya ujenzi wa tenki kubwa la kuhifadhia maji huko Salasala jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Modester Mushi kaimu mkurugenzi wa ufundi DAWASA.
 Hapi na msafara wake wakipanda juu ya tanki linalojengwa.
 Mafundi wakiwa kazini huko Salasala.
Hapi akipokelewa na Meneja Uhusiano wa Jamii, DAWASA, Nelly Msuya, wakati akiwasili huko Makongo Juu, kuanza ziara ya kukagua miradi hiyo.
 Meneja Uhusiano wa Jamii, Nelly Msuya, (wapilia kushoto) na Afisa Uhusiano wa Jamii wa DAWASA, Mecky Mdakju, wakimsubiri Mkuu wa wilaya Mhe. Hapi, alipozuru eneo la Makongo Juu kukagua ujenzi wa kituo cha kusukuma maji.
Hapi, (kulia), akifurahia jambo na afisa kutoka DAWASCO,Judith Singinika(katikati), baada ya kutembelea eneo la ujenzi Bunju.
 Tenki kubwa likifunikwa huko Salasala.
Hapi, (kushoto), akiwa na Modester Mushi kaimu mkurugenzi wa ufundi DAWASA, (kulia) na Nelly Msuya, Meneja Uhusiano wa Jamii, DAWASA, walipotembelea ujenzi wa kituo cha kusukuma maji Bunju.
 Mkuu wa wilaya akizungumza na vibarua.

 Mkuu wa Wilaya  Hapi, akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa ziara hiyo, huko Mabwepande.
Mecky Mdaku, Afisa Uhusiano wa Jamii, DAWASA, akipanda juu ya tenki la Makongo Juu lililofikia asilimia 80 kukamilika
Posted by MROKI On Saturday, January 13, 2018 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo