Watanzania wameshauriwa kupenda kununua bidhaa zinazozalishwa nchini ili waweze kukuza soko la ndani na uchumi kwa ujumla.
Hayo yamesemwa na Meneja Masoko, Tafiti na Maendeleo wa BANK OF AFRICA (BOA), Muganyizi Bisheko, wakati alipokua akikabidhi msaada wa vyerehani kwa Chuo Cha Mafunzo ya Ufundi kilichopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Alisema ili uchumi wa nchi wanchi ukue haraka, watanzania wanapaswa kubadili mitazamo ya kudhani kuwa bidhaa za nje ni bora kuliko bidhaa za ndani, jambo ambalo si sahihi.
Alisema katika kipindi hiki cha sayansi na teknolojia, Watanzania wengi wamepiga hatua katika uboreshaji wa shughuli zao, jambo ambalo limechangia kuwepo kwa bidhaa bora zinakubalika katika soko la ndani nan je ya nchi.
“ ifike wakati Watanzania tunapaswa kubadili mitazamo yetu na kuamini kuwa, bidhaa zinazozalishwa nchini zina ubora unaokubalika, jambo ambalo linachangia kupata masoko ya ndani na njke ya nchi”, alisema Bisheko.
Alisema Benki hiyo inashirikiana na wadau mbalimbali wakiwamo wamiliki wa vyuo na viwanda vidogo ili kuhakikisha wanaboresha shughuli zao na kujiongezea kipato.
Naye Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Oystebay, Sister Getrude Amandus, alisema chuo hicho kinatoa mafunzo ya ufundi ili kuwawezesha vijana kujiajiri.
Meneja Masoko, Tafiti na Maendeleo wa BANK OF AFRICA (BOA), Muganyizi Bisheko, akikabidhi msaada wa vyerehani kwa Chuo Cha Mafunzo ya Ufundi kilichnopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment