NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
MATUMIZI
bora ya bonde la Mto Pangani, ndio njia pekee itakayosaidia kutunza vyanzo vya
maji ambayo hutumika kuzalisha umeme kwenye vituo vya Pangani Hydro Systems,
Meneja wa vituo hivyo, Mhandisi Mahenda S Mahenda amewaambia wahariri wa vyombo
vya habari wanaotembelea bwawa la Nyumba ya Mungu lililoko mpakani mwa wilaya
ya Mwanga na Simanjiro.
“Tanesco
kama wadau wakubwa wa Mto huu, tumeona Mto umeingia mchanga na mchanga huo unatakiwa
kuondolewa ili kuweza kuzalisha maji mengi zaidi kutoka bwawa la Nyumba ya
Mungu na maji hayo yaweze kupatikana kwenye vituo na hatimaye kuzalisha umeme
kama ambavyo inatakiwa.” Alisema Mhandisi Mahenda.
Pangani
Hydro Systems ni mkusanyiko wa vituo vitatu vya kufua umeme vinavyofuatana
ambavyo vimejengwa sehemu tofauti tofauti katika Mto Pangani.
Vituo
hivyo ni pamoja na Nyumba ya Mungu, kituo cha Hale na kituo cha New Pangani
Falls na vyote kwa ujumla wake huzalisha umeme wa Megawati 97 ambazo huingizwa
kwenye Gridi ya Taifa, alisema Mhandisi Mahenda.
Kituo
cha Nyumba ya Mungu, kilizinduliwa mwaka 1964 na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu
Nyerere, na kina mashine mbili za kufua umeme zilizofungwa tangu mwaka huo na
kila moja inao uwezo wa kuzalisha Megawati 4 za Umeme na kufanya jumla ya Megawati
8
Hata
hivyo changamoto kubwa inayokikabili kituo hicho na vituo vingine ambavyo vyote
huendeshwa kwa kutumia nguvu za maji, ni mabadiliko ya tabia nchi na ongezeko
la shughuli za kibinadamu kandokando ya Mto huo pamoja na kwenye bwawa lenyewe
na hivyo kupelekea upungufu wa mara kwa mara wa maji ya kutosha kuendesha
mitambo.
“Tunashirikiana
na wenzetu wanaosimamia bonde la Mto Pangani, kwa kufanya doria za mara kwa
mara ili kuwaelimisha wananchi matumizi bora na endelevu ya maji ya Mto huo ili
kuleta manufaa kwa pande zote, amesema Mhandisi Mahenda.
Mhandisi Mahenda S. Mahenda(kulia), akifafanua mambo mbalimbali kwa wahariri kwenye bwawa la Nyumba ya Mungu Desemba 19, 2017
0 comments:
Post a Comment