Nafasi Ya Matangazo

December 01, 2017

Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Mgambo katika Kata ya Mhange, Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma.
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
VIJANA  waliohitimu mafunzo ya Jeshi la akiba (Mgambo) katika Kata ya Mhange wilayani Kakonko mkoani Kigoma wametakiwa  kuyatumia mafunzo yao katika kukabiliana na vitendo vya uvunjifu wa amani katika jamii.

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala ,wakati akifunga mafunzo ya mgambo katika Kata ya Mhange ambapo jumlanya vijana 84 wamehitimu mafunzo yao.

Kanali Ndagala alisema kumekuwa na matukio mbalimbali ya kiharifu yanayotokea hasa ukilinganisha na kata hiyo kiwa karibu na Nchi jirani ya Burundi hivyo ni vyema vijana hao kutumia mafunzo yao katika kuimarisha usalama ndani ya kata hao.

"Ningependa kuona mafunzo yenu yanakuwa chachu ya kuimarisha ulinzi na usalama kwenye maeneo yenu msiende kuwa sehemu ya waharifu na kuharibu dhima ya kuwa na mafunzo ya mgambo nitarajie kuona amani,uwajibikaji,na mambo mengine ya mafanikio yakifanyika katika maeneo yenu ili wananchi waweze kufanya shughuli zao kwa usalama na kuendelea kuinua uchumi wa Wanakakonko",alisema Mkuu huyo.

Aidha aliwaomba kushirikiana na Wananchi kuwaibua watu wanaokodisha Mashamba kwa Warundi  hali inayoweza kusababisha uharifu kuongezeaka kutokana na tabia ya baadhi ya Wananchi kushirikiana na Warundi, kwani mafunzo waliyoyapata ni kwaajili ya kulinda Amani na usalama wa Watanzania, na kusimamia usalama wa mali za Wananchi na kuweka usalama wa Wananchi.

Hata hivyo aliwaasa Vijana hao kuunda vikundi vya ujasiliamali kabla ya kupata ajira kwakuwa sasa ni muda wa kufanya kazi na kufanya kazi kwa ushirikiano ilikuweza kukuza vipato vyao kwa kuungana na inapotokea kazi za ulinzi wataonwa na kupewa kipaumbele na kujitahidi kuwa waaminifu.

Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi mmoja wa wahitimu hao Sarah  Katunzi  alisema licha ya kufikia hatua hiyo wapo baadhi ambao walishindwa kufikia mwisho wa mafunzo yao na hii nikutokana na mwitikio mdogo kwa baadhi ya wazazi kuwazuia watoto wao wasishiriki mafunzo hayo.

 Alisema mafunzo hayo yamewafanya kuwa wakakamavu na watu wanaopenda kazi na kuwaomba wazazi kuendelea kuwahimiza watoto wao ambao wapo Nyumbani hawana kazi wajiunge na jeshi la akiba iliwawe wazarendo na kujijengea uwezo wa kujiajiri.
Posted by MROKI On Friday, December 01, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo