NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
MKUU
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya
Kikwete, (pichani juu), ameongoza mahafali ya kumi (10), ya Chuo kikuu kishiriki cha Elimu (DUCE) cha
Chuo kikuu Dar es salaam kwenye viwanja vya chuo hicho, Chang’ombe jijini Dar
es Salaam leo Novemba 15, 2017.
Katika mahafali hayo zaidi ya wanachuo 1,443 waliochukua mafunzo ya Shahada ya Elimu ya Jamii na Elimu, (BAED), Shahada ya Elimu ya Sayansi na Elimu, (Bsc) na Shahada ya Elimu (BED), pamoja na wahitimu waliojiendeleza (Post graduate), walitunukiwa shahada ya
kwanza, ambapo mwanachuo Dadi Omary Safari, alipewa tuzo ya kuwa mwanachuo
bora zaidi kitaaluma.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, akimpongeza mmoja wa wahitimu wa Shahada ya Elimu ya Jamii na Elimu, (BAED) Amisa Hassan. |
Baadhi ya wahitimu katika mahafali ya 10 ya ya Chuo kikuu kishiriki cha Elimu (DUCE) cha
Chuo kikuu Dar es salaamwakiwa kwenye mahafali hayo
Furahaya kuhitimu na kutunukiwa shahada.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala, akisoma hotuba yake.
Dkt. Kikwete, akipitia ratiba ya mahafali hayo.
Dkt. Kikwete akitangaza kuwatunuku shahada baadhi ya wanachuo hao. |
Baadhi ya wanachuo wakisubiri kutunukiwa shahada zao na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete.
Dkt. Kikwete, akiteta jambo na Profesa Mukandala.
Dkt. Kikwete, akiipitia tuzo ya mwanachuo bora kitaaluma Dadi Emmanuel Safari kabla ya kumkabidhi.
Mwanachho bora kitaaluma Dadi Emmanuel Safari akiwa na tuzo yake.
Dkt. Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mmoja wa wahitimu, Amisa Hassan, na baba mdogo wa muhitiumu huyo, Khalfan Said.
0 comments:
Post a Comment