Waziri wa
Fedha na Mipango Mhe. Phillip Mpango akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa
tawi la benki ya TPB Mto wa Mbu. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
ya TPB Profesa Lettice Rutashobya. Uzinduzi wa tawi hilo la Mto wa Mbu
ulifanyika jana huko Mto wa Mbu, Arusha.
Waziri wa
Fedha na Mipango Dr. Philip Mpango akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa
mfanyakazi wa benki ya TPB Ignas Mkawe, mara baada ya uzinduzi wa tawi la benki
hiyo hulo Mto wa Mbu, Mkoani Arusha. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo
Sabasaba Moshingi.
Mwenyekiti
wa Bodi ya TPB Bank Profesa Lettice Rutashobya, akikabidhi zawadi ya ngao kwa, Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Philip Mpango, kwenye hafla ya uzinduzi wa
tawi la benki hiyo lililopo Mto wa Mbu Arusha. Akitazama ni Afisa Mtendaji Mkuu
wa Benki hiyo Sabasaba Moshingi.
Waziri wa
Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango akitoa zawadi kwa mmoja wa wateja,
Ester Mfuru, wa tawi la Benki ya TPB huko Mto wa Mbu, wakati wa uzinduzi wa
tawi hili. Kutoka kushoto ni Meneja wa tawi hilo Selestine Mteta na Mkuu wa
Wilaya ya Monduli Mhe. Idd Kimanta. Kulia ni Afisa Mtendaji wa Benki ya TPB
Sabasaba Moshingi na Mwenyekiti wa Bodi ya TPB Prof. Lettice Rutashobya.BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Mgeni rasmi
kwenye uzinduzi wa tawi jipya la Benki ya TPB Mhe. Dkt. Philip Mpango (c) akiwa
kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi waandamizi wa benki hiyo. Kutoka
kulia waliokaa ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Sabasaba Moshigi na Mwenyekiti
wa Bodi ya Benki hiyo Profesa Lettice Rutashaobya. Kushoto ni Meneja wa tawi
hilo Selestine Mteta na Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Idd Kimanta. Waliosimama
nyuma ni baadhi ya viongozi waandamizi wa benki hiyo.
****************
BENKI ya TPB
imeendelea kusogeza huduma zao karibu zaidi na wateja kwa kufungua tawi jipya Mto wa Mbu, Wilayani Monduli, Mkoani
Arusha.
Lengo la
kufungua tawi hilo ni kusogeza huduma za kibenki karibu zaidi na wananchi na
wao kupata fursa ya kutoa huduma kwenye mazingira bora na ya kisasa zaidi, ili
wakazi wa mkoa huo waendelea kufaidika na huduma bora zenye gharama nafuu.
Akizungumza
wakati wa kuzindua tawi hilo, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya TPB, Profesa
Lettice Rutashobya alisema tawi hilo jipya litaongeza idadi ya wateja kwenye
benki yao.
Alisema pia
wananchi wa Arusha, watafaidika na mikopo mbalimbali inayotolewa na TPB
inayokidhi mahitaji ya vikundi, wafanyabiashara wadogo na wakubwa, mikopo ya
wafanyakazi na hata wastaafu.
‘Ni matumaini
yangu kuwa tawi hili litaongeza idadi ya wateja watakaofika kupata huduma
mbalimbali tunazozitoa, kwani TPB tunatoa huduma bora na zenye kukidhi matakwa
ya kila mwananchi katika jamii ikiwemo mikopo kwa vikundi visivyo rasmi,’
alisema Profesa Rutashobya.
Alisema kwa
sasa lengo lao kubwa ni kuendelea kutoa huduma bora zaidi ili kuwanufaisha
wananchi wa kipato cha chini.
‘TPB
inaendelea na jitihada zake za kupeleka huduma za kibenki karibu zaidi na
wananchi kwani mbali na kufungua tawi hili, mwazoni mwa mwaka jana tulifungua
matawi katika Mkoa wa Ruvuma, Kilimanjaro na Babati mkoani Manyara,’ alisema.
Kwa upande
wake mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip
Mpango alisema serikali itakuwa bega kwa bega na TPB kutokana na jitihada zake
za kupeleka huduma karibu zaidi na wananchi kwa kutumia teknolojia ya kisasa na
hata mawakala.
‘Mimi binafsi
na serikali tumekuwa mstari wa mbele kuhakikisha taasisi za kifedha nchini
zinatoa msukumo unaotakiwa katika shughuli za kiuchumi nchini, ikiwemo
kuwawezesha wazalishaji kuboresha
ufanisi na tija kwa mambo ya msingi katika ukuaji wa uchumi,’ alisema.
Alisema pia
serikali itaendelea kutoa msukumo kwa sekta za kibenki pamoja na zingine juu ya
umuhimu wa kutumia teknolojia ya kisasa katika uzalishaji na utoaji wa huduma
kwa kuamini kwamba teknolojia bora huwezesha
kuboresha ufanisi, kupunguza gharama na kupanua wigo wa soko.
Naye Meneja
wa TPB tawi la Mto wa Mbu, Selestine Mteta alizitaka taasisi mbalimbali
vikiwemo vyuo, mashirika na hata shule kufungua akaunti za taasisi na TPB ili
kupata huduma za kisasa na zenye gharama nafuu.
0 comments:
Post a Comment