Shirikisho
la ngumi Tanzania (BFT) limeanda mashindano ya ngumi yaliyofanyika tarehe
30/09/2017 kati ya timu yaTaifa ya Ngumi dhidi ya timu ya Ngome inayomilikiwa
na Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) Mashindano hayo yalikuwa ni jaribio la kwanza
kwa timu yetu ya ngumi inayoendelea na mazoezo kwa ajili ya maandalizi ya
kushiriki Mashindano ya Jumuiya ya Madola yatakayofanyika Gold Coast, AUSTRALIA
Aprili 2018.
Na yalikuwa pia na lengo la uzinduzi rasmi wa mazoezi ya kujiandaa na
mashindano hayo.
Mashindano
hayo ya siku moja yalifunguliwa na Mkurugenzi wa michezo Tanzania ndugu Yusuph
Singo.
Timu hiyo ya
Taifa iliyo na mabondia wa kiume na kike imeanza vema jaribio hilo la
kwanza baada ya kushinda michezo tisa
dhidi ya mitatu walioshinda Ngome kwa upande wa wanaume baada ya kuwa mazoezini
tangu mwanzoni mwa mwezi wa nane 2018.
Kwa upande
wa mabondia wa kike wote walioshiriki ni kutoka timu ya Taifa.
Matokeo
yalikuwa kama ifuatavyo:-
WANAUME,
1 .
Herman
Shekivuli (Taifa) alimshinda Issa Kpaya (Ngome) 49 Kgs.
2.
Geoge
Costantino (Taifa) alimshinda John
Christian (Ngome) 52 Kgs
3.
Ezra
Paul (Taifa) alimshinda Emmanuel Marwa ( Ngome) 56 Kgs
4.
Ismail
Galiatana (Taifa) alimshinda Fabian Gaudence (Ngome) 60 Kgs
5.
Mohameda
Juma (Taifa) alimshinda Isiaka Lusajo (Taifa) 64 Kgs
6.
Kassim
Butike (Taifa) alimshinda Julius Nickson (Ngome) 69 Kgs
7.
Selemani
Kidunda (Taifa) alimshinda Daudi Kuzenza (Ngome) 75 Kgs
8.
Yusuph
Changarawe (Taifa) alimshinda Twalibu Kinyogori (Ngome) 81 Kgs
9.
Haruna
Swanga (Taifa) alimshinda Alex Sitta (Taifa)
10.
Alex
Michael Ngome) alimshinda Mwalimu Ngayana (Taifa)
11. Kelvin
Kapinga (Ngome) alimshinda Said Ramadhani ( Taifa)
12. Batele
Abed (Ngome ) alimshinda Mwinyi Ally (Huru)
WANAWAKE
1.
Siwatu
Kimbe (Taifa) alimshinda Lusiana Gadani (Taifa)
2.
Safina
Fussi (Taifa) alimshinda Asha Juma (Taifa)
3.
Najma
Isike (Taifa) alimshinda Monica Malango (Taifa)
4.
Mariam
Macho (Taifa) alimshinda Naomi Shoo Taifa)
5.
Grace
Mwakamale (Taifa) alimshinda Leonia Kalimunju ( Taifa)
Aidha wakati
wa kufungua mashindano hayo Mkurugenzi wa michezo Yusuph Singo alisema serikali
imeona na inatambua jitihada zinazofanywa na BFT katika kuendeleza mchezo wa Ngumi
Tanzania na hasa hatua za kuandaa timu ya Taifa mapema kwa ajili ya kushiriki
mashindano ya Jumuiya ya Madola 2018.
Alisema serikali
itakuwa karibu na BFT kuhakikisha mazoezi hayo yanaendelea vizuri na kusaidiana
kuondoa changamoto zilizopo.
Alieleza
kuwa kwa hivi sasa serikali ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha mpango wa
timu ya Taifa ya ngumi kwenda nchini Cuba kwa ajili ya mazoezi ya kushiriki
mashindano ya Jumuya ya madola 2018.
Mwisho BFT
imeahidi kuwa mashindano hayo yatakuwa yanafanyika kila wa kila mwezi kwa kushindana na timu za ndani na nje
ya Tanzania.
Taarifa hizi
zinaletwa kwena na
0 comments:
Post a Comment