Nafasi Ya Matangazo

October 25, 2017

 Katibu tawala wa wilaya ya Iringa Joseph Chintinka akiwa kwenye mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Iringa manispaa akizungumza na baadhi ya walimu walihudhuria mkutano huo. 
Baadhi ya walimu waliokuwa wanaimba wimbo wa walimu wakati wa mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Iringa manispaa uliofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu huria tawi la Iringa.

Na Fredy Mgunda,iringa. 

Walimu wa halmashauri ya manispaa ya Iringa wametakiwa kutumia kondomu ili kujikinga na magonjwa ya zinaa amboya yamekuwa yakipunguza nguvu kazi ya taifa.

Hayo yamesemwa na katibu tawala wa wilaya ya Iringa Joseph Chintinka wakati wa mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Iringa manispaa.

Chintinka alisema kuwa kumekuwa na ongezeko la waathirika wa ugonjwa wa ukimwai kutokana na kufanya mapenzi bila kutumia kondomu.

“Jamani hapa Iringa kuna tatizo kubwa la ugonjwa wa ukimwi hivyo niwaombe walimu wangu tutumie kondomu ili kujiepusha na gonjwa hili vinginevyo vizazi vyetu vyote vitaambukizwa ukimwi” alisema Chintinka

Chintinka alisema njia ya kuwa salaama kuepukana na gonjwa hili ni kujikinga kwa kutumia kondomu maana hata watoto wetu wameathirika kutokana na wazazi kutokuwa makini na matumizi ya kinga

“Naombeni tuwakinge hawa watoto wetu ambao wameathirika ili wasiwaambukize watoto wengine maana bila hivyo tutakuwa na kizazi kilichoathirika” alisema Chintinka

Aidha Chintinka aliwaomba walimu walioathirika kujitokeza ili kupewa lishe ambayo inatolewa na serikali bure hivyo walimu wametakiwa kujitokeza na kuweka wazi kwa mwagili wake ili aweze kupata mgao wa pesa za lishe.

“Jamani walimu fungu la lishe kwa walimu walioathirikia ni nono kweli naombeni walimu mjitokeze ili mfaidi fungu hili nono maana mimi nafahamu sisi ndio tunaotenga naombeni fikisheni ujumbe huu kwa walimu wengine ambao hawajafika hapa” alisema Chintinka

Chintinka aliwataka watumishi wanaotoa siri za watumishi walioathirika kuacha tabia hiyo mara moja ili kuwaweka huru waathirika na wengine waweze kujitokeza na wapate lishe iliyotengwa na wilaya.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama hicho manispaa ya Iringa MWL. Zawadi Mgongolwa alikiri kuwepo kwa viongozi wa sekta hiyo ambao wemekuwa wakitoa siri za walimu na watumishi walioathirika na ugonjwa wa ukimwi.

Kwa kweli mgeni rasmi umeongea ukweli kero kubwa kwa walimu ni kutolea siri nje kitu kinachowafanya walimu waathirika kujificha na maradhi yao” alisema Mgongolwa

Naye katibu wa chama cha walimu wilaya ya Iringa mwl. Fortunata Njalale alimpongeza mgeni rasmi kwa ujumbe wake ambao umekuwa faraja kwa walimu na kuwaongezea hali ya kwenda kufanya kazi ya uwalimu kwa kujituma na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wao.


Posted by MROKI On Wednesday, October 25, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo