Nafasi Ya Matangazo

July 07, 2017


Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka wa Udhibiti wa Manunuzi ya Umma  PPRA Dkt Laurent Shirima akizungumza na wanahabari wakati alipotembelea banda la Mamlaka wa Udhibiti wa Manunuzi ya Umma PPRA lililopo kwenye jengo la Wizara ya Fedha na Mipango na kuelezea namna wanavyojizatiti katika kuboresha ununuaji wa zabuni kwa serikali.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka wa Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Dkt Laurent Shirima akimuhudumia mwananchi aliyetembelea banda lao na katika maadhimisho ya 41 ya Monesho ya kimataifa ya Sabasaba leo Jijini Dar es salaam.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka wa Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Dkt Laurent Shirima akipata maelezo kutoka kwa  mfanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa Taifa (PPF) wakati alipotembelea banda hilo lilipo katika Jengo la Wizara ya Fedha na Mipango  katika maadhimisho ya  41 ya Monesho ya kimataifa ya Sabasaba leo Jijini Dar es salaam.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka wa Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Dkt Laurent Shirima  akisaini katika kitabu cha wageni wa Wizara ya Fedha na Mipango alipotembelea banda hilo katika maadhimisho ya 41 ya Monesho ya kimataifa ya Sabasaba leo Jijini Dar es salaam.
Afisa Mahusiano Mwandamizi wa Mamlaka wa Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Mcharo Mrutu akimuhudumia mwananchi aliyetembelea banda lao katika maadhimisho ya  41 ya Monesho ya kimataifa ya Sabasaba leo Jijini Dar es salaam
Mtaalamu wa Mifumo ya Habari wa Mamlaka wa Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Mapinduzi Muhochi akitoa elimu ya manunuzi ya zabuni kwa mwananchi aliyejitembelea  banda lao  katika maadhimisho ya  41 ya Monesho ya kimataifa ya Sabasaba leo Jijini Dar es salaam. Picha Zote na Emannuel Massaka.
*************
 MAMLAKA  wa Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA)imejizatiti kwa kufanya marekebisho ya sheria ikiwa ni katika kuboresha zaidi manunuzi ya bidhaa na vifaa kwa serikali.

Akizungumza wakati akitembelea banda la PPRA lililopo kwenye jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Dkt Laurent Shirima amesema kuwa maboresho hayo yatalenga katika sehemu tano ambazo zitaboresha manunuzi ya zabuni katika nyanja mbalimbali.

Dkt Shirima amesema kuwa sheria hiyo imeboreshwa katika kupunguza gharama za ununuaji wa Bidhaa na vifaa, serikali kununua kwa bei za sokoni wakimaanisha bei halisi ya bidhaa na vifaa pia wametoa upendeleo kwa makampuni ya ndani ikiwemo makundi maalumu kama vile wanawake, wazee na vijana.

Ameongezea kuwa, katika maboresho mengine yaliyofanywa ni katika kuendeleza viwanda kama serikali ya awamu ya tano inavyosisitiza ukuaji wa viwanda huku PPRA ikiangalia zaidi wataalamu wa manunuzi kutoka ndani pia wapo katika hatua za mwisho za kuhamia katika mfumo wa kieletroniki wa ununuzi wa zabuni.

PPRA ni mamlaka inayohusiana na udhibiti wa manunuzi ya Umma ambapo kupitia kwa Mtendaji Mkuu Dkt Shirima amewaondoa hofu wananchi kuwa waiamini taasisi yao kwani mambo mengi ya msingi yameshawekwa wazi na fedha za umma zinahitaji uwajibikaji.
Posted by MROKI On Friday, July 07, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo