Muonekano wa Daraja la
Kavuu lenye urefu wa Mita 89 linalounganisha Halmashauri ya Wilaya ya Mlele na Halmashauri ya Wilaya ya Mpwimbwe
Mkoani Katavi ambalo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99.
Meneja Wa Wakala Wa
Barabara nchini (TANROADS), Eng. Abdon Maregesi (kulia), akitoa maelezo kwa
Naibu Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Katikati) juu
ya hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Daraja la Kivuu wakati Naibu Waziri huyo
alipokagua, Mkoani Katavi.
Naibu Waziri Wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa kwanza kushoto),
akikagua ujenzi wa Nyumba za viongozi zinazojengwa na Wakala Wa Majengo nchini
(TBA) Mkoani Katavi, Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mlele Bi. Rachel
Kassanda.
Naibu Waziri Wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akiongea na wananchi wa
kata ya MajiMoto Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi mara baada ya kukagua Daraja la
Kavuu ambalo ujenzi wake umekamilika na linatarajiwa kuanza kutumika mwishoni
mwa mwezi huu. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI.
Naibu Waziri Wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akisalimiana na wakazi wa
kata ya MajiMoto Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi mara baada ya kuongea nao.
Naibu Waziri Wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Kulia) akiongea na Mbunge
wa Jimbo la Manyoni Magharibi, Omary Yahya Massare (Kulia), Wakati Waziri
Ngonyani alipotembelea Jimboni kwake mwishoni mwa wiki.
******************
Ujenzi wa Daraja la
Kavuu lenye urefu wa Mita 89 linalounganisha Halmashauri ya Wilaya ya Mlele na Halmashauri ya Wilaya ya Mpwimbwe
Mkoani Katavi ujenzi wake umekamilika na litaanza kutumika ifikapo mwishoni mwa
mwezi Julai mwaka huu.
Akizungumza mara baada
ya kukagua ujenzi wa Daraja hilo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amesema kukamilika kwa ujenzi huo kutarahisisha
usafirishaji wa abiria na Mizigo kutoka
Mkoa wa katavi kwenda mikoa ya jirani.
“Serikali iliona kero kubwa
wanazozipata wananchi wa mkoa huu hasa kwenye usafirishaji wa abiria na mizigo
kwenye kipindi cha mavuno, hivyo baada ya kukamilisha Daraja hili wananchi
wataweza kupita vipindi vyote vya Mwaka,” alisema Naibu Waziri Eng. Ngonyani.
Aidha, Eng. Ngonyani
amemuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Katavi Eng. Abdon
Maregesi Kuhakikisha Mzani unaohamishika unawekwa ili kudhibiti magari
yatakayozidisha Tani 36.
Kwa upande wake Meneja
wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Katavi Eng. Abdon Maregesi amemuhakikisha Naibu
Waziri, Eng. Ngonyani kuwa wakala utaweka mzani huo ili kutoruhusu magari
yaliyozidisha Uzito wa Mzigo kupita kwenye Daraja hilo.
Wakati huo huo, Naibu Waziri
Eng. Ngonyani amekagua ujenzi wa Nyumba za Viongozi Mkoani humo na kuuagiza
Wakala wa Majengo nchini (TBA), kuhakikisha ujenzi wa nyumba hizo unakamilika ifikapo Novemba
mwaka huu.
“Serikali imeshatoa
fedha za kukamilisha ujenzi wa nyumba hizi, ujenzi huu ulisimama kwa takribani
miezi minne kwa sasa hakuna sababu ya ujenzi kusuasua wakati fedha zipo,
ninakuhakikishia Mkuu wa Wilaya nyumba hizi zitakamilika kwa wakati ili zianze
kutumika,” alisisitiza Naibu Waziri Eng. Ngonyani.
Katika hatua nyingine
Naibu Waziri Eng. Nyonyani amekagua ujenzi wa Barabara ya Sitalike-Mpanda yenye
urefu wa kilomita 36.9 ambao ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99, barabara
hii ni sehemu ya barabara kuu inayoanzia Tunduma kupitia Sumbawanga, Mpanda,
Uvinza, Kibondo, Nyakanazazi hadi Mutukula.
Naibu Waziri Eng.
Ngonyani yupo katika Ziara ya kukagua Miundombinu ya barabara, Viwanja vya
Ndege, Ujenzi wa Nyumba za viongozi na Madaraja katika Mkoa wa Katavi.
0 comments:
Post a Comment