Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi TAMISEMI, Elisa Rwamiago akielezea kuhusu mfumo wa kielektroniki katika ujazaji taarifa za fedha katika vituo vya kutolea huduma.
Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi TAMISEMI, Elisa Rwamiago akizungumza ukumbini.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Bwana Elizeus Rwezaula akizungumza ukumbini
Mkuu wa Idara ya Ufuatiliaji,Tathmini na Tafiti Tendaji kutoka PS3, Dkt. Suma Kaare akizungumza ukumbini ambapo alisema mfumo wa ujazaji taarifa kwa njia ya kielektroniki ulibuniwa na PS3 kisha kuwasiliana na serikali ambayo kwa pamoja wameamua kutekeleza mfumo huo katika halmashauri mbalimbali nchini
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo akijifunza kwa vitendo jinsi ya kuingiza taarifa za fedha kwa njia ya kielektroniki
Washiriki wa mafunzo hayo wakijifunza kwa vitendo namna ya kujaza taarifa za fedha kwa kutumia kompyuta
Mwenyekiti wa mafunzo hayo ya FFARS ,Samson William akizungumza ukumbini wakati akiendesha majadiliano mbalimbali
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano PS3, Leah Mwainyekule akielezea utaratibu utakaotumika kwa wakufunzi waliopata mafunzo ya FFARS watakavyokwenda kutoka elimu kuhusu FFARS katika vituo vya kutolea huduma
Kabla ya kufundishwa njia ya kieletroniki katika kujaza taarifa za fedha,washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika kikundi wakijadili namna ya kujaza taarifa kwa njia ya zamani ya kutumia vitabu.Walijadili namna ya kutunza kumbukumbu za miamala ya kifedha na nyaraka kwa kutumia vitabu
Washiriki wakiendelea na kazi ya vikundi.Washiriki hao walijifunza pia namna ya kuandika miamala ya kifedha kwenye nyaraka na vitabu vya uhasibu.
********************
WAHASIBU zaidi
ya 130 kutoka Halmashauri za Wilaya kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kati wameanza kupatiwa
mafunzo ya Mfumo wa Kielekroniki kuhusu Usimamizi wa fedha ngazi za msingi
zikiwemo Zahanati,vituo vya Afya,Hospitali na Shule za Msingi na Sekondari.
Mafunzo
hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha
kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and
Reporting System’ ( FFARS) kupitia mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za
Umma ‘ Public Sector Systems Strengthening – PS3’ unaotarajiwa kuanza kutumika
Julai 1,2017 katika halmashauri mbalimbali nchini.
Wahasibu
hao wanashiriki katika mafunzo yanayofanyika katika ukumbi wa Vigimark Hotel
Mjini Shinyanga ambayo yamekutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi
kutoka PS3,TAMISEMI,Wizara ya afya,wizara ya elimu.
Mwezeshaji
wa Mafunzo hayo, Elizeus Rwezaula ambaye ni Mshauri wa Masuala ya Usimamizi wa
Fedha za Umma kutoka Mradi wa HPSS Dodoma,alisema mfumo wa kutumia njia za
kielektroniki (kompyuta) katika kuingiza taarifa za kifedha za vituo vya
kutolea huduma unasaidia kurahisisha kazi.
“Katika
Afrika Mashariki,Tanzania ndiyo nchi pekee itakayoanza kutumia mfumo huu wa
kisasa wa kielektroniki katika uingizaji taarifa za fedha katika ngazi za msingi
za kutolea huduma,na umetengezwa na vijana wa hapa nchini ili kuhakikisha kuwa
mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea
huduma (FFARS) unafanikiwa”,alieleza Rwezaula.
“Tunawashauri
wale wanaoendelea kutumia mfumo wa zamani wa ujazaji taarifa kwa kutumia vitabu
(manual) waanze kutumia mfumo huu mpya wa uingizaji taarifa kwa mfumo wa
kompyuta ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia”,aliongeza
Rwezaula.
Kwa upande
Mkuu wa Idara ya Ufuatiliaji,Tathmini na Tafiti Tendaji kutoka PS3, Dk. Suma
Kaare alisema mfumo wa ujazaji taarifa kwa njia ya kieletroniki ulipendekezwa
na PS3 na tayari serikali imeukubali na utaanza kutekeleza mwezi Julai,2017
katika halmashauri mbalimbali.
Naye Afisa
Msimamizi wa Fedha Mwandamizi TAMISEMI, Elisa Rwamiago alisema baada ya
wahasibu hao kupatiwa mafunzo kuhufu FFARS nao wataenda kutoa elimu kuhusu
mfumo kwa watoa huduma wengine wa ngazi za chini.
0 comments:
Post a Comment