Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Rehema Madenge akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mafunzo kwa Maofisa Habari na Maofisa Tehama wa Halmashauri na Mikoa ya Dodoma, Singida, Iringa, Geita, Pwani, Manyara na Dar es Salaam chini ya Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Mjini Dodoma. Mafunzo hayo yanahusu uanzishaji na uendeshaji wa Tovuti za Serikali. Na Mroki Mroki/Daily News-Habarileo Digital.
Kiongozi wa Habari na
Mawasiliano PS 3, Leah Mwainyekule akitoa maelezo ya mradi huo unaofa ambapo alisema Mradi wa
Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya
Kimataifa la Marekani (USAID)ujulikanao kwa Kiingereza kama Public
Sector Systems Strengthening (PS3) ni wa miaka mitano, na
utafanya kazi na
Serikali Kuu pamoja na Halmashauri 93 katika mikoa 13 ya Tanzania bara.
Ila katika uboreshaji wa mawasiliano kwa umma mradi huo unashirikisha
Halmashauri na mikoa yote ya Tanzania bara kwa kuwapa mafunzo maafisa
habari na maafisa Tehama wa maeneo husika.
PS3 inalenga kuunda
ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya sekta za
umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa
taarifa, na tafiti tendaji. Ushirkiano huu wa PS3 katika ngazi ya Serikali kuu
na Halmashauri, una nia ya kukuza utoaji, ubora, na matumizi ya huduma za umma,
hususan kwa jamii ambazo hazijanufaika vya kutosha.
Washiriki wa mafunzo hayo ambao ni Maofisa Habari na Maofisa Tehama kutoka Mikoa na Halmashauri mbalimbali kutoka mikoa ya Dodoma, Singida, Iringa, Geita, Pwani, Manyara na Dar es Salaamwakifuatilia mafunzo hayo. BOFYA HAPA KUONA ZAIDI.
Mgeni Rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Rehema Madenge akiwa na Kiongozi wa Mawasiliano wa Mradi wa PS3, Leah Mwainyekule wakifuatilia mada.
Mwezeshaji kutoka PS3, Donald Samwel akitoa mada ya juu ya Tovuti za serikali na uendeshaji wake.
Washiriki wa mafunzo hayo ambao ni Maofisa Habari na Maofisa Tehama kutoka Mikoa na Halmashauri mbalimbali kutoka mikoa ya Dodoma, Singida, Iringa, Geita, Pwani, Manyara na Dar es Salaamwakifuatilia mafunzo hayo.
Ofisa Habari wa Serikali Mtandao (eGA), Rainer Budodi akitoa mada wakati wa mafunzo hayo juu ya namna bora ya uendeshaji tovuti za serikali na ni vitu gani vinapaswa kuchapishwa.
Washiriki wa mafunzo hayo ambao ni Maofisa Habari na Maofisa Tehama kutoka Mikoa na Halmashauri mbalimbali kutoka mikoa ya Dodoma, Singida, Iringa, Geita, Pwani, Manyara na Dar es Salaamwakifuatilia mafunzo hayo.
Picha mbalimbali za pamoja zilipigwa kati ya meza kuu na washiriki. Source: www.dailynewstzonline.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment