Na Bety Alex, Arusha
JESHI la polisi kwa mkoa wa arusha limefanikiwa kukamata bunduki 10 pamoja na
risasi 59 ambazo zilikuwa zinatumika kwenye matukio mbalimbali ya uhalifu
Risasi 59 ambazo zilikuwa
zinatumika na wananchi wa maeneo ya Ngorongoro mkoani Arusha na taarifa
za awali zinaonesha kuwa zilikuwa zinatumika kwenye ujangili.
Akiongea
na vyombo vya habari mapema leo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charlz Mkumbo alisema kuwa kunaswa kwa silaha hizo kunatokana na oparesheni
iliyofanyika kwa zaidi ya wiki mbili nakuhusisha maeneo mbalimbali mkoani Arusha.
Mkumbo amesema kuwa katika kijiji chaMagaiduru Kata ya Olorien Tarafa ya Loliondo silaha aina ya Chinese 56 smg yenye namba MT .70 B 1
2730021 ikiwa na magazine yenye risasi 21 ilikutwa
katika ofisi ya kijiji baada ya kutelekezwa na mtu asiyejulikana .
Ameongeza kuwa katika kijiji cha Oldonyosambu ilipatikana
silaha aina ya mark 1V yenye namba ZKK 5602 iliyotelekezwa kwenye
kichaka ambapo katika kijiji cha jema kata ya oldonyosambu
askari waliokuwa katika operesheni hiyo walifanikiwa kupata silaha nne
aina ya Chinese 56 smg pamoja na risasi 19.
Katika hatua nyingine kamanda amedai kuwa muwemdelezo wa operesheni hiyo
ulizidi kufanikisha kupata silaha tatu katika kijiji cha Sale Tarafa ya Sale ambazo ni Chinese 56 SMG yenye namba 89020539 ikiwa na risasi 15
pamoja na S.A.R yenye namba 263126 zilipatikana na hivyo kusababisha
operesheni hiyo kukamata jumla ya silaha kumi za aina nne tofauti pamoja
na risasi 59.
Hataivyo jeshi hilo mkoani hapa limetoa onyo kali kwa wakazi
wote wa arusha wanaomiliki silaha kinyume cha sheria wazisalimishe mara
moja katika ofisi za mtaa au kijiji kwani watakuwa katika mkono salama
na atakayekaidi amri hii hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi
yake.
0 comments:
Post a Comment