Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango (kulia) akizindua nembo mpya na jina jipya la iliyokuwa Benki ya Posta Tanzania na sasa inajulikana kama TPB Bank Plc, ikiwa ni mabadilko yaliyofanywa
baada ya benki hiyo mwaka jana kuorodheshwa chini ya sheria ya makampuni.
Benki hiyo ambayo ina miaka 92 tangu kuanzishwa
kwake, ilibadilishwa uendeshaji wake baada ya mwaka 2015, Bunge kufuta sheria
iliyoanzisha benki hiyo na kuifanya kuwa kampuni ili kusajiliwa chini ya Sheria
ya Makampuni, mchakato uliokamilika mwishoni mwa mwaka jana na kwa sasa inaitwa
TPB Bank Plc.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Bank, Sabasaba Moshingi akizungumza wakati wa uzinduzi wa jina hilo jipya na nembo ya Benki hiyo Dar es Salaam leo.
Moshingi
alisema mabadiliko hayo yanakwenda sanjari na mabadililo makubwa ndani ya benki
hiyo.
“Benki iliamua kubadilisha nembo ili kwenda
sambamba na jina hilo na mabadiliko ya
kuboresha benki ili yanayoendelea,” alisema Moshingi na kuongeza kuwa kwa sasa
wako katika mchakato wa kujiorodhesha kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam
(DSE) na kuwa ni fursa ya Watanzania kununua hisa katika benki hiyo ambayo
faida yake imekuwa ikikua kila wakati.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, TPB Bank, Profesa Lettice Rutashobya akizungumza.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, akizungumza na kuipongeza TPB Bank kwa hatua iliyofikia na kusema kuwa serikali iko katika mikakati ya kuhakikisha nchi inafikia uchumi wa
viwanda ifikapo mwaka 2025, na kuwa sekta ya fedha ambayo inakuwa kwa kasi ina
mchango mkubwa katika kufikia azma hiyo. BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI.
Alisema serikali ambayo inamiliki benki hiyo kwa
asilimia kubwa, ingependa kuiona faida ya uwekezaji wake kwa uongozi
kuhakikisha wanapelekahuduma zao katika kusaidia sekta ya viwanda kwa kutoa mikopo.
Mmoja wa Maofisa wa TPB Bank akielezea nemba mpya ya benki hiyo na maana yake.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango akimpongeza
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, TPB Bank, Profesa Lettice Rutashobya
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, TPB Bank, Profesa Lettice Rutashobya
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (katikati) akiwa na Afisa Mtendaji wa Tpb Bank, Sabasaba Moshingi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki hiyo, Prof.Lettice Rutashobya wakifurahia mabadiliko na jina ;la iliyo kuwa benki ya Posta Tanzania ambayo jana Waziri Mpango alizindua jina na nembo mpya.
Meza kuuu ikifuatilia matukio.
Wafanyakazi na wageni mbalimbali waalikwa wakifuatilia matukio.
Mgeni rasmi alipewa zawadi ya saa ya Ukutani iliyo na nembo mpya ya TPB Bank. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango akipokea kadi ya TPB popote kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo.
Wafanyakazi wakifuatilia matukio na kusikiliza hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa.
Picha mbalimbali za pamoja pia zilipigwa.
0 comments:
Post a Comment