Mkurugenzi
wa Ufundi wa Soka la vijana TFF, Kim Paulsen akitoa maelekezo kwa
wachezaji wa timu ya vijana U-17 wakati wa ufunguzi wa kliniki ya Airtel
Rising Stars katika uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam jana.
Kliniki
ya Soka ya Airtel Rising Stars imeanza leo kwenye Uwanja wa Karume kwa
kuwakutanisha wavulana 40 na huku ya wasichana ikifanyika kwenye uwanja
wa JK Park zamani kidongo chekundu.
Akizungumza
wakati wa kliniki hiyo, Kocha Mkuu wa Timu ya Serengeti Boys, Bakari
Shime alisema, ‘kwanza tutakuwa tukiangalia ufundi binafsi wa mchezaji’.
Hii ni mara ya kwanza kukutana na wachezaji hawa na kuangalia vitu
binfasi ambavyo mchezaji anatakiwa kuwa navyo hii itatusaidia kujua ni
sehemu ipi ya kutilia mkazo.
Juhudi
binafsi za Mchezaji, Ufundi na stamina (ukakamavu) ni vitu muhimu kwa
mchezaji kuwa navyo katika kiliniki hii, hiyo ndio sababu leo kwa siku
ya kwanza wachezaji tumewapa nafasi ya kuchezea mpira ili kuangalia vitu
hivyo,’ alisema Shime.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano
akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa kliniki ya
Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam jana.
Lakini
pia tutapata nafasi ya kuingalia timu yetu ye Serengeti Boys kama ina
mapungufu yoyote na kama kutakuwa na wachezaji wenye umri mkubwa basi
hauwaruhusiwa kuendelea kuchezea timu ya vijana.
Hapa
ndipo tutapa fursa ya wachezaji wa kuweza kuziba nafasi zilizoachwa wazi
katika timu hiyo, Kwa wiki hii yote tutakuwa na kazi ya kushirikiana
na Makocha wengine kuikamilisha zoezi hili, aliongeza Shime.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Maendeleo ya Soka la vijana TF, Ayoub Nyenzi
alisema, ‘klikini ya Airtel Rising Stars inatoa fursa pana kwa vijana
chipukizi kuonyesha uwezo wao mbele ya makocha wenye uzoefu wa mpira wa
miguu nchini’.
Katibu
Mkuu TFF, Selestine Mwesigwa akizungumza na waandishi wa habari wakati
wa ufunguzi wa kliniki ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Karume
jijini Dar es Salaam jana.
Hii ni
nafasi adhimu kwa vijana wetu kuendelea kuonyesha uwezo wao na kuzidi
kuendeleza vipaji vyao. Sio lazima wachezaji wote hawa hawawezi
kuchanguliwa kuchezea timu ya vijana ya Serengeti Boys, lakini kuna
klabu zetu ambazo zinaitahitaji wachezaji kwenye timu zao za vijana. Hii
ndio nafasi kwao kujitokeza na kuangalia wachezaji wenye uwezo wa
kuchezea timu zao, Ayoub aliyasema hayo jana.
Naye
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya
alisema, ‘kufanyika kwa kliniki ya Airtel Rising Stars kunahitimisha
awamu ya sita ya michuano ya Airtel Rising Stars’ ambayo ilifanyika kwa
Mikoa tisa nchini kwa mafanikio makubwa sana.
‘Nachukua
fursa hii kuwashukuru TFF pamoja na wadau wote wa mpira wa miguu nchini
ambao tumeshirikiana kwenye 2016 Airtel Rising Stars. Michuano hii
lifanyika kwa mafanikio makubwa sana na leo tunapaonza kliniki hii
inayojumuisha wachezaji bora naomba tuendelea tushirikiana kwa pamoja
ili vijana wetu waweze kutimiza ndoto zao za kuwa wachezaji bora katika
maisha yao’ alisema Mallya
0 comments:
Post a Comment