Mkurugenzi Mkuu, Mh. James Kilaba
Na Mwandishi Maalum, Hammamet,
Tunisia
PAMOJA na maendeleo na faida
mbalimbali za Tekinolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), masuala ya
Usalama, faragha na imani katika matumizi bado yameendelea kuwa masuala ya
kuwekwa maanani katika ngazi za kitaifa na kimataifa.
Akihutubia kikao cha Mkutano wa
Dunia wa Masuala ya Viwango Katika Mawasiliano (World Telecommunication Standardization
Assembly – WTSA-16) mjini Jasmine
Hammamet, nchini Tunisia hivi karibuni, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA), Eng. James Kilaba amesema tekinolojia mpya ndani
ya TEHAMA zina mchango mkubwa katika
usalama (wa mitandao,mifumo, vifaa, data na
wa watumiaji); faragha ( katika data na watumiaji) na Imani (kwenye
mitandao,mifumo, vifaa, data na kwa
watumiaji).
“Katika vikao kama hivi vya
majadiliano kuhusu TEHAMA, wakati mwingi hatusahau kuzungumzia masuala ya
huduma, vifaa na ukuaji wa watumiaji, mtandao na hata mapato. Leo
tunazungumzia mchango wa teknolojia mpya
katika usalama, faragha na Imani katika matumizi ya TEHAMA”, Mkurugenzi Mkuu wa
TCRA aliuambia mkutano huo.
Eng. Kilaba ailisema kumekuwepo
na mabadiliko ya teknolojia kutoka zilizotawaliwa kwa kiasi kikubwa na
kuendeshwa kwenye mfumo wa intaneti kwa kutumia kompyuta binafsi zilizounganishwa
kwa mfumo wa waya hadi tekinolojia zinazotumia vifaa ya mkononi
vilivyounganishwa bila kutumia waya. Amesema hii imewezesha na kufanikisha
mawasiliano zaidi na kwa kupitia mfumo wa intaneti kuifikia dunia
iliyounganishwa na mfumo wa kompyuta.
Eng Kilaba aliongeza kwamba mada
kuu ya majadioiano katika mkutano huo ilikuwa ni huduma, vifaa, kukua na
kuongezeka kwa watumiaji na kupanuka na kwa mifumo ya mawasiliano ambayo
inawafika mbali zaidi na kuwafikia watu wengi zaidi.
“Wasimamizi wa mawasiliano duniano
kote wanayo changamoto ya kukabiliana na mahitaji ya watumiaji na kubadilika
kwa vifaa, bila kujali kuwa vimefungwa wapi au kutumiwa vipi ili mradi
vinaimarisha usalama, faragha na Imani ya watumiaji. Kwa hiyo kimsingi ni watu
ambao wanaishi kwenye utamaduni tofauti na katika maeneo tofauti ya
kijiografia”, amesema Mkurugenzi Mku wa TCRA.
Ameeleza kwamba Tanzania, kama
nchi inayoendelea imefanya mengi katika sekta ya usalama wa mitandao ya
kompyuta zinazotumika kwa mawasiliano. Aliongeza kwamba Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania inao mfumo wa Usalama wa Matumizi ya Usalama Mtandaoni ambao umewekwa
kwa kushirikisha wadau mbalimbali.
Amesema Tanzania imeanzisha mfumo
wa kitaifa wa kushughilikia dharua zinazohusiana na matumizi ya kompyuta za
mawasiliano (TZ- CERT) ambao unatumika kutoa elimu kuhusu masuala ya usalama wa
mitandao, taarifa na ujuzi kwa wadau na watumiaji ili kuwawezesha kuwa na
kiwango cha kuridhisha cha utaalamu
unaohitajika katika kushughulikia masuala makubwa yanayohusiana na matumiai ya
mitandao ya inayotumia mifumo ya kompyuta kwa mawasiliano.
Hali kadhalika, aliongeza kuwa Tanzania
ina kituo cha kitaifa kinachohifadhi data. Vilevile aliuambia mkutanio huo
kwamba Tanzania imeanzisha utaratibu wa kuzuia matumizi mabaya ya data au taarifa
kutoka kwenye simu za mkononi zilizoibwa nchini Tanzania.
Eng. Kilaba alisema kwamba
vitengo vya kushughulikia dharua za mifumo ya mawasiliano inayotumia kompyuta
imeanzishwa katika nchi nne na kwa kiasi kikubwa nchi hizo zinabadilishana na
kulinganisha taarifa kuhusu masuala ya usalama wa mitandao.
Kupitia umoja wa taasisi za Mawasiliano
Afrika Mashariki ambao unajulikana kama EACO, nchi wanachama zinakutana na
kujadili masuala mbalimbali kuhusu usalama wa mitandao. Aliongeza kwamba
changamoto zilizojitokeza kuhusiana na usalama, faragha na Imani katika
matumizi ya TEHAMA zinaweza kuainishwa katika maeneo matano ambao ni viwango
hafifu, sera, sheria na mikakati.
“Viwango, Sheria na Mikakati
vinahitajika ili kuinua kiwango cha ulinzi wa nchi katika masuala ya ulinzi wa
mitandao. Kwa kuwa masuala ya usalama wa mitandao hayaishii ndani ya mipaka ya
ncchi moja, viwango vilivyowekwa, sheria zilizowekwa na Kanuni zilizopo
znahitajika kuhuishwa ili zitumike
katika maeneo ya nchi zaidi ya moja na pia ulimwenguni pote. Inaaminika kwamba
kuna wataalamu wachache wa masuala ya usalama wa mitandao wenye hadhi ya
kimataifa wanaoweza kushughulikia kikamilifu ulinzi na makosa yanayohusiana na
mitandao” alileza Mhandisi Kilaba.
Alisisitiza kwamba kuna umuhimu
wa kuwa na mikakati ya kitaifa kuhusu masuala ya usalama wa mitandaoo ambayo
itawezesha kueneza elimu, ufahamu na ujuzi wa watumiaji na wadau wengine na
watumiaji wengine ili kuwawezesha kushughulikia kikamilifu matukio ya usalama
wa mitandao. Alisema kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na mfumo wa kuthibiti usalama
wa mitandao ndani na nje ya mipaka ya nchi husika.
“Baadhi ya nchi zinazoendelea
hazina mifumo ya kuthibiti usalama wa mitandao ya kompyuta za mawasiliano.
Mifumo hii ikiwekwa na kutumika
inawezesha uratibu, uchambuzi na uchukuaji wa hatua za kuimarisha mifumo
na kubadilishana taarifa kuhusu usalama na tishio kwa mifumo ya kompyuta za mawasiliano’, Eng.
Kilaba aliuambia mkutano huo.
Mkutano wa WTSA unafanyika kila
baada ya miaka minne. Mkutano wa wa
mwaka huu ulianza 25 Oktoba hadi Novemba
3. Ulitanguliwa na Mkutano wa Dunia wa
masuala ya viwango uliofanyika 25 Oktoba
2016.
0 comments:
Post a Comment