Makamu wa
Rais , Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya
uchunguzi wa saratani ya matiti pamoja na ya mlango wa kizazi kwenye uwanja wa
Furahisha jijini Mwanza.
Makamu wa
Rais wa, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalim (katikati) pamoja na Mwenyekiti wa
Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania Dk. Serafina Mkuwa wakati wa uzinduzi wa
kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti pamoja na ya mlango wa kizazi kwenye
uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.
Makamu wa
Rais, Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia
,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalim kwenye moja ya mabanda yaliokuwa yanatoa
huduma wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti pamoja
na ya mlango wa kizazi kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.
Makamu wa
Rais, Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi waliojitokeza wakati wa
uzinduzi wa kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti pamoja na ya mlango wa
uzazi kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.
Sehemu ya
Wanawake waliojitokeza kwennye uzinduzi huo.
****************
Makamu wa
Rais , Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wananchi kuwa serikali imeweka
mipango na mikakati thabiti ya kukabiliana na idadi kubwa ya vifo
vinasababishwa na saratani hasa saratani
ya matiti na mlango wa kizazi kote nchini. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Makamu wa
Rais Samia ametoa kauli hiyo katika viwanja vya furahisha jijini Mwanza
wakati akizundua kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti na mabadiliko ya
awali ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani humo.
Katika
hotuba yake kwa mamia ya wananchi wa mkoa wa Mwanza waliojitokeza katika
uzinduzi huo, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania ikiwa ni nchi
mojawapo Kusini mwa Jangwa la Sahara ina kiwango cha juu cha vifo vya saratani
ya matiti na mlango wa kizazi ambapo asilimia 60 ya vifo vyote
vinavyotokea Kusini mwa jangwa la Sahara vinasababishwa na saratani
hiyo.
Makamu wa
Rais amesema kuwa vifo vingi vinatokana na uelewa mdogo, imani potofu,gharama
kubwa za matibabu,unyanyapaa na kuwepo kwa vituo vichache wa kufanyia
uchunguzi hapa nchini ambapo kwa sasa tiba ya mionzi inapatikana katika
Taasisi ya Saratani ya Ocean Roas, Dar es Salaam.
Katika
kukabiliana na tatizo hilo, Makamu wa Rais amesema kuwa Wizara ya
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imepokea kiasi cha shilingi
bilioni Tano kutoka Benki ya Dunia fedha ambazo zitawezesha vituo Vitatu kwa
kila Halmashauri ambavyo vitasaidia kuboresha huduma za uchunguzi na matibabu
ya mapema ili wanawake kote nchini hasa wale wale wa vijijini waweze kupata
huduma hizo kwa urahisi na kwa ukaribu kwenye maeneo wanayoishi.
“Wote ni
mashuhuda kwa namna saratani ya mlango wa kizazi inavyosababisha vifo vingi
hali ambayo hutokana na magonjwa wanaogundulika na ugonjwa kuwa tayari
wamefikia hatua isiyotibika na kwa pamoja saratani hizi mbili husababisha zaidi
ya asilimia 50 ya vifo vyote vya akinamama”
Makamu wa
Rais amesisitiza kuwa kwa sasa tayari kuna vituo takribani 300 vinavyotoa
huduma za upimaji wa dalili za awali katika vituo vya afya kote nchini na hivyo
vituo vipya vitaongeza huduma endelevu ili kupunguza vifo vitokanavyo na
saratani.
Makamu wa
Rais pia ametoa wito maalum kwa wanaume kote nchi kuunga mkono kampeni hiyo kwa
kuwaruhusu wanawake na wasichana kwenda kupima saratani hiyo na amewapongeza na
kuwashukuru wanaume wa mkoa wa Mwanza kwa kuwasindika wake zao na watoto wao wa
kike kwenda kwenye vituo vya afya kwa ajili ya kupima saratani hiyo na kupatiwa
tiba.
Makamu wa
Rais amepongeza Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania- MEWATA na wadau wote kwa
kuanda zoezi la huduma za uchunguzi wa dalili za awali za saratani ya mlango wa
kizazi.
Kwa upande
wake, Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye wagonjwa wengi wa
saratani ya mlango wa kizazi na pia ndiyo inaongoza katika nchi za Afrika
mashariki.
Amesema
kuwa idadi ya wanawake 6241 hugundulika kuwa na saratani kila mwaka na
kati yao zaidi ya nusu yaani 4355 hufariki dunia. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
0 comments:
Post a Comment