Na Bety Alex, FK Blog -Arusha
VILIO na majonzi vimetawala katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha baada ya Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbles Lema
kulazimika kwenda mahabusu katika gereza kuu la Kisongo kutokana na
kuwekewa pingamizi la dhamana.
Hatua hiyo imekuja baada ya wanasheria wa serikali
wakiongozwa na Maternus Marandu na Paulo Kadushi kupinga dhamana ya Mbunge huyo kutokana na kile walichodai akipewa dhamana ataendelea
kufanya mikutano ya uchochezi.
Pia waliieleza Mahakama hiyo mbele ya hakimu Desderi
Kamugisha kuwa uchunguzi wa kesi zingine za uchochezi zinazomkabili
alipatiwa dhamana kwa lengo la kujikerebisha lakini ameendela kukiuka
utaratibu wa dhamana ambapo alipaswa asifanye tena makosa yanayofanana
kila mara
Kwa upande wa mawakili wa upande wa mhishatakiwa
wakiongozwa na John Mallya na Ahmed hamisi ,sheck mfinanga pamoja na
charles adieli walisema kuwa mshtakiwa ana haki ya kupata dhamana kwa
sababu ni haki ya msingi na kisheria na kesi zinazomkabili bado
hazijafanyiwa hukumu hivyo ana haki ya kupata dhamana bila kukiuka
taratibu nq sheria za nchi. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Walisema kuwa mshitakiwa ni mbunge wa kuchaguliwa ndani ya
jamhuri ya tanzania mbapo ana2akilisha wananchi hivyo ni vema mahakama
ikampatia dhamana kwa ajili ya kuendelea na majukumu aliyochaguliwa
nayo.
Mawakili hao walidai pamoja na mbunge huyo kukabiliwa na
kesi mbili za uchochezi namba 440 na 441 za mwaka 2016 ya kutowa
maneno ya lugha ya uchochezi yanayodai nchi hii haitatawalika na
itaingia kwenye machafuko kama rais hatafuata katiba na sheria bado
wanaamini makosa hayo yanastahili kupata dhamana kama sheria ya makosa
ya mwenendo ya jjnai.
Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili hakimu
kamugisha alihairisha shauri hilo hadi november 11 itakapokuja kutolewa
uamuzi mdogo huku mshitakiwa lema akirejeshwa rumande katika gereza la
kisongo kusubiri hatma ya dhamana yake
Wakati mbunge huyo akiondoshwa mahakamani hapo akiwa chini
ya ulinzi mkali wa polisi alionekana kujiamini na kushika biblia
takatifu akiwa kwenye gari la polisi ambapo ndipo wafuasi hao walianza
kuangua kilio wakimlialia mbunge huyo huku wengine wakizimia.
Kufuatia tukio hilo mwenyekiti wa chama cha demokrasi na
maendeleo mkoani hapa Amani Golugwa aliwaomba wananchi wa arusha kuwa
wavumilivu katika kipindi hiki wakati shauri hilo likiwa mahakamani na
kujitokeza kwa wingi kufuatilia kesi hiho.
Awali kabla ya kusikilizwa kwa kesi hiyo mahakama kuu kanda
ya arusha chini ya jaji Salma magimbi alimuamuru mwanasheria wa
serikali awe amemleta mshitakiwa ndani ya nusu saa mahakamini hapo baada
ya kukaa mahabusu ya polisi kwa zaidi ya masaa 175 kinyume cha sheria
ya mwenendo ya makosa jinai.
Hata hivyo kabla ya amri ya mahakama hiyo polisi walimleta
mshitakiwa katika mahakama hiyo majira ya saa mbili asubui na hivyo
kurahisisha amri ya mahakama hiyo
0 comments:
Post a Comment