Nafasi Ya Matangazo

February 20, 2026








Na Mwandishi Wetu,
 Morogoro
Elimu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia imeendelea kuwafikia wananchi katika soko la Mahindi na vijiwe vya bodaboda waliopo Mikese Morogoro  lengo likiwa ni kuhakikisha watu wanaachana na matumizi ya nishati isiyo safi ya kupikia kama vile kuni na mkaa.

Wizara ya Nishati kwa kushirikiana na Mfuko wa Maendeleo ya Mitaji wa Umoja wa Mataifa (UNCDF) inaendelea na  kampeni endelevu ya nishati safi ya kupikia  ambapo tarehe 19 Februari 2026 kampeni hiyo iliwafikia wananchi katika Kata ya Mikese, wilaya ya Morogoro vijijini.

 Timu ya uhamasishaji imekuwa ikizungumza na wananchi na wafanyabiashara ili kubaini nishati wanayotumia na kuwapatia elimu ya umuhimu wa kuhamia katika nishati safi.

Baadhi ya wananchi wameeleza kuwa wanahitaji kutumia gesi zaidi wanapopika hivyo wameomba Serikali kuweka gharama rafiki  za ununuzi wa nishati hiyo.
Posted by MROKI On Friday, February 20, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo