MKUU wa Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma Luice
Bura (wapili kulia) akiangalia moja ya mashimo ya vyoo ambayo hayajamaliziwa ujenzi wake.
MKUU wa Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma Luice
Bura (katikati) akizungumza wakati wa ukaguzi.
Na FK Blog-Kigoma
MKUU wa Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma Luice
Bura amemtaka Kurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kibondo kuwasimamisha kazi
watumishi watatu katika kitengo cha ujenzi kwa tuhumaa za ubadhirifu wa
fedha kiasi cha Sh Milioni 109.
Fedha hizo ni sehemu ya Sh milioni 264 zilizotakiwa
kumaliza mradi wa vyumba vitatu vya madarasa na nyumba ya walimu yenye uwezo wa
kuishi familia za watu sita na matundu matano ya vyoo katika
Sekondari ya Itaba katani humo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Maagizo hayo aliyatoa jana katika kikao cha
ulinzi Na usalama ambacho yeye ndiye Mwenyekiti wa kamati hiyo baada ya kufika
eneo la Ujenzi wa vyumba vya madarasa Na vyoo katika shule za Sekondari Tank na Nyumba za walimu Na kukuta vyoo havija sakafiwa Na vyumba
vingine havijajengwa.
Bura aliwataja watumishi watakao simamishwa ni
pamoja na Salehe Mbogoye, Felix Ngomano na Haruni Mbapaye kutoka idara ya
ujenzi , ambao ndio waliokuwa wakisimamia ujenzi wa majengo hayo na kuchangia
upotevu wa sh.milioni 109, ilihali kiasi cha sh.milioni 46 zimelipwa
bila kufanyiwa kazi na ujenzi uliofanyika upo chini ya kiwango huku ujenzi
upo chini ya asilimia 50%
na kuidhinisha malipo hewa.
" baada ya
kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi kutokana na mradi huo
niliamua kuituma Kamati ya ulinzi na usalama ,walifika katika eneo la ujenzi na
kukuta ujenzi haujakamilika ambapo matundu ya choo ni mashimo
tu, madirisha hayapo sakafu haijawekwa na ninakuomba Mkurugenzi
uwasimamishe kwa muda watumishi hao hadI uchunguzi utakapo kamilika kutokana Na
tuhuma hizo",alisema Bura.
Hata hivyo Bura alisema cha kushangaza Madiwani
wa kamati ya ujenzi waliomba posho ya kufanya ukaguzi wa
ujenzi na wakapewa posho ya siku tano ,kumbe hata
kwenye eneo la ujenzi hawajafika hali iliyowapelekea watumishi wengine kuangukiwa
na barua za maadili ni pamoja na Ofisa Elimu Sekondari Wilaya
Honolata Kabundugulu, Fedy Eliasafu Ofisa Maliasili na Ofisa kilimo wilaya Said
Shemahonge ambao wataitajika kujibu tuhuma
hizo.
Akitoa ufafanuzi juu ya mradi huo Mjumbe wa
kamati ya maendeleo ya kata husika Bosco Ngomagi alisema serikali ihakikishe
inashirikisha wananchi wa eneno husika,ili kuondoa uhujumu uchumi wa jamii
ambapo kamati husika watasimamia mradi husika Na wannchi wtafuatilia kwa
ukaribu ilikujua no kiasi gani kimetengwa ilikuweza kukamilisha mradi Na mradi
ukamilike kwa wakati.
Nao baadhi ya Vibarua kutoka kampuni iliyochukua
zabuni ya ujenzi ya Mangalazi Engenearing ya Kigoma Mjini Paschal
Leonardi walimuomba mkuu huyo awasaidie malipo yao kwa kuwa fedha
nyingi zimeshatumika Na wao hawajapata malipomyao mpakasasa wanaendelea Na kazi
lakini mpakaka sasa kunabaadhi wamechukua fedha hizo bado hawajawalipa.
0 comments:
Post a Comment