WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa amepokea msaada wa Dola za Marekani 33,000 (sawa na sh. milioni
71) kutoka kwa makampuni ya Kuwait ili ziwasaidie
wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera, hivi
karibuni.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi msaada huo leo (Jumatano, Novemba 9, 2016), Balozi wa Kuwait
nchini Tanzania, Bw. Jasem Al-Najem amesema msaada huo ni mchango kutoka kwa Mwenyekiti
wa Umoja wa Makampuni ya Fouad Alghanim, Bw. Fouad Alghanim aishiye Kuwait.
Amesema
watu kadhaa wameguswa na maafa yalitokea mkoani Kagera Septemba 10, mwaka huu na
wameamua kuchangia ili kuisaidia juhudi za Serikali kukabiliana na hali hiyo
ambayo haikutarajiwa.
“Tunatambua
kuwa kazi ya kurejesha huduma kwa wananchi ni kubwa, na Serikali peke yake haiwezi
kubeba mzigo wa kukarabati miundombinu na majengo ya ofisi na makazi ili
kuurejesha mkoa huo katika hali yale ya kawaida,” amesema.
Akizungumza
na Balozi Al-Najem ofisini kwake Bungeni, mjini Dodoma, Waziri Mkuu amesema Serikali
ya Tanzania imeguswa na moyo wa upendo kutoka kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Makampuni ya
Fouad Alghanim na wenzake.
Akitoa shukrani kwa
msaada huo, Waziri Mkuu ameahidi kuwa Serikali itahakikisha mchango huo unafikishwa
Kagera kwa walengwa.
Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani
Kagera, Septemba 10, mwaka huu lilisababisha vifo vya watu 17 na wengine 440
kujeruhiwa. Pia lilisababisha nyumba 2,063 kuanguka huku nyingine 14,081 zikiwa
katika hali hatarishi na 9,471 zikipata uharibifu mdogo huku wananchi 126,315
wakihitaji misaada mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment