SHIRIKA la Ndege la Kitanzania, Precision Air, limezindua
promosheni maalmu kwa ajili ya kuwazawadia wateja wake kuelekea msimu wa
sikukuu. Promosheni hiyo iliyopewa jina la SAFIRI NA USHINDE imezinduliwa jana kupitia mkutano na
waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya shirika hilo.
Kupitia promosheni
hiyo tiketi 100 zitashindaniwa kwa kipindi chote cha promosheni hiyo. Tiketi
hizo zitatolewa kupitia droo zitakazochezeshwa kila wiki kwa wiki kumi
mfululizo, na washindi watajipatia tiketi ya bure kusafiria kwenda popote ndani
ya mtandao wa Precision Air.
Akizungumzia promosheni hiyo, Meneja Masoko na Mawasiliano
Bi. Azda Nkullo amesema, kila abiria na mteja ana nafasi ya kushinda tiketi ya
bure ilimradi tu amesafiri na Precision Air.
“Tunasherekea miaka 23
ya kutoa huduma, na katika kufanya hivyo tutatoa tiketi hizi 100 bure kwa
wateja wetu, kama mkono wa shukrani kwa kuwa pamoja nasi kwa kipindi chote
ambacho tumekua tukitoa huduma.” Aliongeza Bi. Nkullo
Bi. Nkullo ameleza kuwa kwa mteja kushiriki katiko promosheni
hii, anahitajika kununua tiketi ya Precision Air kwenda popote kule ndani ya
mtando wake na kasha kujaza kuponi ya ushiriki wakati wakujisajili na safari na
kuikabidhi kwa muhudumu wakati wakuanza safari.
Tutafanya droo kila Jumatatu ya wiki kwa wiki kumi mfululizo
na kuwatangaza washindi wetu 10 kila wiki. Tunawasihii wateja wetu kuchangamkia
fursaa hii ya kujipatia tiketi ya bure kupitia promosheni hii hasa katika
wakati huu ambapo wanajiandaa na msimu wa sikukuu. Amesisitiz Bi.Nkullo.
Kwa upande wake Meneja Uratibu na Mahusiano Bw. Hillary Mremi
amesema wateja wanaweza kushiriki promosheni hi kwa urahisi kwa kuchangamkia
tiketi za promosheni kupitia tovuti ya Precision Air maarufu kama shavu la
dotcom kwa safari kati ya Dar-Arusha, Dar-Kilimanjaro, Musoma-Mwanza and
Mwanza-Bukoba kwa nauli inayoanzia Sh. 80,000/-
Bw. Hillary Mremi ameongeza pia kuwa tiketi zote zitakazo
nunuliwa kupitia tovuti ya Precision Air zitakua na punguzo la asilimia 10
(10%).
Precision Air
ilianzishwa mnamo mwaka 1993 kama shirika binafsi la ndege za kukodi, ikitumia
ndege ndogo ibebayo abiria wa tano aina Piper Aztec. Katika kuanza kwake
Precision Air ilikua imejikita katika kusafirisha watalii waliokua wakitembelea
vivutio vya utalii nchini (Serengeti, Ngorongoro na Zanzibar) huku makao makuu
yake yakiwa Arusha.
Ikiwa ni miaka 23 ya Precision Air kutoa huduma, Shirika la
ndege la Precision Air limekua na kua moja ya mashirika ya ndege ya
nayoheshimika Africa Mashariki na Africa kwa ujumla.Kwa sasa Shirika hilo
linafanya safari za ndani kuelekea sehemu 11 na safari 2 za kikanda,
likiunganisha abiria kuelekea maeneo mengi zaidi ndani ya Africa na kimataifa.
0 comments:
Post a Comment