Bety Alex,FK Blog-Arusha
Ajali za pikipiki kwa mkoa wa
arusha zimeongezeka mwaka hadi mwaka ambapo mpaka kufikia mwaka 2015 zilifika
ajali 836 huku upande ajali za magari zikipungua kwa asilimia 11.
Hataivyo ajali hizo za
pikipiki kwa mwaka 2010 zilikuwa 709 ukilinganisha na ajali 277 za pikipiki
mwaka 2009 ajali hizo za pikipiki bado zinaendelea kuongezeka.
Hayo yamebainishwa na kamanda
wa kikosi cha usalama barabarani Nuru Selemani wakati akielezea hali ya usalama
wa barabarani kwenye uzinduzi wa maazimisho ya wiki ya usalama barabarani
mapema leo.
Selemani alisema kuwa takwimu
zinaonesha mkoa wa Arusha bado unakabiliwa na ajali za barabarani ambapo kwa
kipindi cha mwaka 2007 ajali zimekuwa zikiongezeka na kulikuwa na ajali 1807na
kufikiakiwango cha juu mwaka 2010 ambapo ajali 2658 huku kwa kipindi cha mwaka
2012 ajali zilianza kupungua hadi kufikia ajali 2011
Alifafanua kuwa baada ya jeshi
kutumia nguvu kubwa sana katika kupunguza ajali zinazotokana na magari
zilipungua sana ingawaje kwa sasa bado wimbi kubwa la ajali linatokana na ajali
za pikipiki.
Katika hatua nyingine alisema
kuwa ajali zinasababishwa na sababu za kibinadamu kwa asilimia 75,madereva
kulewa huku wakiwa wanaendesha vyombo vya moto,pia ubovu wa vyombo vya usafiri
kwa asilimia 15,miundombinu ya barabara kwa asilimia10.
Awali mgeni rasmi katika
uzinduzi huo mkuu wa wilaya ya arusha Fabian Daqaro alisema jukumu la usalama
wa barabarani sio la polisi wenyewe wala kamati ya kikosi cha usalama
barabarani pekee bali ni ulinzi wa kila mtu.
Fabian alisema kuwa endapo
kama kila mtu atafuata sheria na kanuni za barabarani basi ajali zitakuwepo kwa
kiwango cha asilimia 0.0 kwani ajali zinachangia kudidimiza mlengo wa taifa.
Hataivyo katika uzinduzi huo
baadhi ya askari wa usalama barabarani walifanikiwa kupewa vyeti vya ufanyakazi
bora ambapo mmoja wa askari hao Silas Konga alisema kuwa maadili yao bora
kazini yamechangia wao kutambulika na jeshi hilo.
0 comments:
Post a Comment