Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu 2016/17, raundi ya 12
inaendelea keshokwa michezo sita ambako mabingwa watetezi Young Africans
ya Dar es Salaam itakuwa mgeni wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba
ulioko Bukoba mkoani Kagera.
Jijini
Dar es Salaam, katika Uwanja wa Uhuru African Lyon itakuwa mwenyeji wa
Mbeya City ya Mbeya ilihali Mwadui ya Shinyanga itasafiri hadi Mtwara
kucheza na Ndanda Fc kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona wakati Stand
United itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye mchezo
utaofanyika Uwanja wa Manungu, ulioko Turiani – Mvomero.
Majimaji
itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting ya Pwani kwenye Uwanja wa Majimaji
huko Songea. Michezo yote mitano hapo juu itaanza saa 10.00 jioni kwa
saa za Afrika Mashariki lakini mchezo kati ya Azam FC na JKT Ruvu
itaanza saa 1.00 usiku kwenye Uwanja wa Azam huko Chamazi-Mbagala Dar es
Salaam.
Jumapili
itakuwa ni zamu ya kinara wa ligi hiyo, Simba ambayo itaikaribisha Toto
Africans ya Mwanza kwenye Uwanja wa Uhuru wakati Tanzania Prisons
itapambana na Mbao FC kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini
Mbeya.
Michezo
yote ya Dar es Salaam, mfumo wa kuingia utabaki kuwa ni uleule wa
kutumia kadi za Selcom kununua tiketi za kielekroniki. Viingilio kwenye
mechi za Uwanja wa Uhuru ni Sh 30,000 kwa Jukwaa Kuu (VIP-A), VIP-B na C
Sh 20,000 na mzunguko ni Sh 5,000 wakati Kiingilio Uwanja wa Azam ni Sh
10,000 kwa VIP na Mzunguko ni Sh 3,000.
0 comments:
Post a Comment