Nafasi Ya Matangazo

October 21, 2016



Afisa masoko Platinum Credit Tanzania, Gideon Lufunyo (kushoto) akikabidhi msaada wa mifuko 300 ya saruji ambayo ni sawa na tani 15 kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu ikiwa ni msaada wa taasisi hiyo kwa waathirika wa tetemekonla Ardhi mkoani humo.
KAMPUNI ya Platinum Tanzania imetoa msaada wa mifuko 300 ya saruji kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu ,kwa lengo la kusaidia shule zilizoathirika na tetemeko la Ardhi lililotokea hivi Karibu ni.
 
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Afisa masoko wa Platnum Tanzania Gideon Lufunyo alisema wameguswa na janga hilo na kuamua kushirikiana na watanzania mbali mbali kuichangia Kagera.
 
"Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Platinum Tanzania na wafanyakazi wote tunatoa pole kwa mkoa wa Kagera,Rais na watanzania wote kwa ujumla,hili ni janga letu tushirikiane kuhakikisha tunairudisha Kagera yetu katika hali yake ya kawaida,"alisema Lufunyo.
 
Akipokea msaada huo Mkuu wa mkoa huo aliishukuru Platinum kwa msaada huo na kwamba wameupeleka kipindi ambacho unahitajika.
Posted by MROKI On Friday, October 21, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo