Nafasi Ya Matangazo

October 17, 2016

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Devis Deogratius akiongea na  mawakala na wageni waalikwa


Mfanyabiashara  Julius  Masalu mkazi wa Mwanza (katikati) akipokea funguo za gari alilojishindia katika droo ya promosheni ya Nunua,Uza ,Shinda na Konyagi iliyohusisha mawakala wa kuuza bidhaa za kampuni ya Tanzania Distillers Ltd (TDL) kutoka kwa Meneja wa Chapa ya Konyagi,Martha Bangu (Kulia),anayeshuhudia kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TDL,Devis Deogratius. Droo ya pili ya promosheni hiyo ilifanyika  mwishoni mwa wiki katika viwanja vya hoteli ya Kili Home mjini Moshi mwishoni mwa wiki ikihusisha washiriki 31 kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini na kanda ya ziwa.Mfanyabiashara  Julius  Masalu mkazi wa Mwanza (katikati) akipokea funguo za gari alilojishindia katika droo ya promosheni ya Nunua,Uza ,Shinda na Konyagi iliyohusisha mawakala wa kuuza bidhaa za kampuni ya Tanzania Distillers Ltd (TDL) kutoka kwa Meneja wa Chapa ya Konyagi,Martha Bangu (Kulia). Droo ya pili ya promosheni hiyo ilifanyika  mwishoni mwa wiki katika viwanja vya hoteli ya Kili Home mjini Moshi mwishoni mwa wiki ikihusisha washiriki 31 kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini na kanda ya ziwa.Mawakala wa Konyagi wakiserebuka wakati wa hafla hiyo.
Meneja Masoko wa TDL,George Kavishe akiwashukuru mawakala walioshiriki kwenye promosheni hiyo
MFANYABIASHARA  Julius  Masalu (58) mkazi wa Mwanza ameibuka mshidi wa gari aina ya Eicher lenye thamani ya shilingi milioni  56  katika mzunguko wa pili wa bahati nasibu ya Promosheni ya  Nunua,Uza ,Shinda na Konyagi iliyohusisha mawakala wa kuuza bidhaa za kampuni ya Tanzania Distillers Ltd (TDL).

Droo ya pili ya promosheni hiyo ilifanyika  katika viwanja vya hoteli ya Kili Home mjini Moshi mwihoni mwa wiki ikihusisha washiriki 31 kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini na kanda ya ziwa na kusimamiwa na afisa wa Bodi ya Taifa ya michezo ya kubahatisha Humudi Abdul Hussein.

 Akiongea kwa furaha baada ya kutangazwa kuwa mshindi, Masalu alisema ametoka Mwanza akiamini kuwa atajishindia gari hilo na kwamba bahati nasibu hiyo imeendeshwa kwa uwazi na hakuna upendeleo unaoweza kufanyika.

 “Katika bahati nasibu hii hakuna  longo longo,shindano limeendeshwa kwa uwazi mkubwa sana na namshukuru Mungu kwa kuweza kupata zawadi hii ya gari itanisaidia sana katika kusambaza bidhaa za  kampuni  ya konyagi kwa wateja wangu,” alisema Masalu.

 Kaimu Meneja  Mkuu wa Konyagi, Devis  Deogratius alisema dhumuni ya promosheni hiyo ni  kukuza uhusiano wa kibiashara na wasambazaji wa bidhaa za TDL pamoja na kuwapatia kifaa kitakachosaidia katika kupanua masoko ,kusambaza na kuongeza ufanisi.

 “Safari ilianza mwezi wa saba hadi mwezi wa tisa ,kumekuwa na usawa katika mchakato huu wa kumpata mshindi na hakuna upendeleo wowote ,wale ambao wamefikia malengo wamefika katika promosheni hii  na kuwepo hali ya usawa katika kushinda zawadi ya gari”alisema Deogratius.Alisema mbali na mshindi huyo wa gari  katika droo hii ya kwanza washiriki  watano walibahatika  kujishindia katoni 10 za Konyagi kila mmoja.

 Baadhi ya washiriki katika droo hiyo, Mkamba Zephania na Joas Muganyizi  walisema wameridhishwa na mchakato mzima ulivyofanyika katika kuchezesha droo na wala hapakuwa na kasoro ama udanganyifu wowote.

 “Kampuni ya TDL kupitia bidhaa yake ya Konyagi katika promosheni ya Nunua  Uza,Shinda na Konyagi imesaidia kuwakutanisha wafanyabiashara wa maeneo mengine ya kanda ya Kaskazini na kanda ya ziwa hali inayochangia kuongeza wigo katika kufanya biashara”.Alisema Muganyizi.

Washindi wengine waliojinyakulia katoni 10 kila mmoja za bidhaa ya Konyagi na maeneo wanayotoka kwenye mabano ni pamoja na Linus Mathew (Kagera) Msemo Enterprises (Arusha) ,Joace Muganyizi(Bukoba) Mkamba Zephania (Bariadi) na Yohana Masunga (Geita).

Huu ni mzunguko wa pili wa droo ya bahati nasibu ya Promosheni ya Nunua Uza,shinda na Konyagi ambapo katika droo ya kwanza mfanyabiashara Grace Oroki,  mkazi wa Jijini Dar es salaam, alijinyakulia gari kwa mawakala wa kuuza bidhaa za kampuni ya TDL wa mikoa ya Nyanda za juu Kusini na Pwani.
Posted by MROKI On Monday, October 17, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo