Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wapili kulia) akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mugombe wilayani Kasulu. Kulia ni Mbunge wa Kasulu, Daniel Nsanzugwanko na kulia kwa Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Martin Mkisi.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Martin Mkisi akizungumza na wananchi wakati wa Ziara ya Waziri wa
Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo.
Waziri wa
Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo akizungumza na wananchi.
*************
WANANCHI wa Wilaya ya Kasulu
Mkoani Kigoma, wanataraji kuanza kufaidi umeme wa REA pindi awamu ya pili ya
mradi huo itakapo kamilika mwishoni mwa Octoba 2016.
Hayo yamesemwa na Waziri wa
Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo, alipotembelea miundombinu ya Umeme wa
REA katika Wilaya ya Kasulu.
Waziri Muhongo yupo katika
ziara ya siku tano mkoani Kigoma kuangalia utekelezaji wa awamu ya pili ya
miradi ya REA mkoani humo na Wilayani Kasulu aliongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo
Kanali Martin Mkisi.
Prof Muhongo, akiambatana na
Wahandisi wa Tanesco, REA na Wakandarasi wanaojenga miundombinu hiyo,
wamezungumza na wananchi katika kijiji cha Mugombe na Heru Juu Wilayani Kasulu.
Aidha katika awamu ya tatu, vijiji vipatavyo
29 vitakamilishiwa huduma hiyo muhimu kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya
ya Kasulu, Kanali Martin Mkisi, amewataka wananchi kutunza miundombinu ya
umeme, kuchangamkia fursa za kufunga umeme wa bei rahisi na kujitokeza kwa
wingi kwenye mafunzo yatakayotolewa na
Tanesco kuhusu umeme wa REA.
Pia amewaagiza wakandarasi
kukamilisha usambazaji wa huduma hiyo ifikapo Octoba 30 mwaka huu bila kuongeza
siku hata moja.
0 comments:
Post a Comment