Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akisalimiana na Kamishna wa Tume ya Sekretarieti ya Maadili ya Umma Jaji Mstaafu Salome
Kaganda mara baada ya kuwasili kwenye halfa fupi ya uzinduzi wa jengo la
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kusini mkoani
Mtwara
Jengo la
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kusini mkoani
Mtwara
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akihutubia wakati wa halfa fupi ya uzinduzi wa jengo la
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kusini mkoani
Mtwara
Kamishna wa Tume ya Sekretarieti ya Maadili ya Umma Jaji Mstaafu Salome
Kagandaakihutubia kwenye hafla hiyo
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Ofisi ya Rais Menejimenti Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki akihutubia kwenye hafla hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa jengo la
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kusini mkoani
Mtwara
*************
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameiagiza
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Nchi kuchunguza na kuwachukulia
hatua kisheria na za kinidhamu viongozi na watumishi wa umma ambao wanakiuka
taratibu za kazi kwa ajili ya maslahi yao binafsi.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 8-Sep-2016 mjini Mtwara wakati anafungua jengo la sekretarieti ya
maadili ya viongozi wa umma Kanda ya Kusini ambalo ujenzi wake umegharimu
takribani shilingi Bilioni mbili.
Makamu
wa Rais amesema iwapo kama hatua hizo zitachukuliwa haraka zitakomesha na
kupunguza kasi ya mmomonyoko wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma hali
ambayo itaongeza uwajibikaji katika utendaji wa kazi miongoni watendaji hao.
Amesisitiza
kuwa serikali itaendelea kuiimarisha sekretarieti ya maadili ya viongozi wa
umma nchini kwa kuijengea uwezo wa rasilimali watu na fedha kwa kadri hali ya uchumi
itakavyo ruhusu ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Makamu
wa Rais amewahimiza viongozi na watumishi wa umma kuthamini na wahakikishe
walinda maslahi ya umma wakati wote wa utendaji wao wa kazi ili kuondoa
malalamiko kwa wananchi.
Makamu
wa Rais amesema ni jambo la muhimu kwa sekretarieti hiyo kufutilia mienendo ya
viongozi wa umma na kuwabaini wale wanaokwenda kinyume na misingi ya uadilifu
na wachukuliwe hatua ipasavyo kabla hawaleta madhara kwa serikali na jamii kwa
ujumla.
Makamu
wa Rais pia ametoa rai maalum kwa wananchi wa mkoa wa Mtwara kuitumia ofisi
hiyo mpya ya sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma Kanda ya Kusini kwa
kutoa taarifa kuhusu mienendo ya viongozi wanaokiuka maadili ya umma katika
utendaji wao wa kazi ili waweze kuchukuliwa hatua.
Kwa
upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala bora Angela Kairuki amesisitiza kuwa kazi ya kuhakiki mali na madeni ya
viongozi wa umma itaendelea kwa kasi nchini na mwaka huu sekretarieti hiyo
itahakiki mali za viongozi wapatao 500 kote nchini.
Naye
Jaji Mstaafu na Kamishna wa Maadili Nchini Salome Kaganda akitoa taarifa kuhusu
ujenzi wa jengo hilo ameiomba serikali itenge fedha za kutosha kwa ajili ya
kufanikisha zoezi la uhakiki wa mali na madeni ya viongozi kwa nchi nzima.
0 comments:
Post a Comment