Gwaride la wahitimu wa mafunzo ya kijeshi kwa askari na maafisa wa Hifadhi za Taifa likiingia katika viwanja vya mazoezi katika kambi ya mafunzo ya Mlele wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na
Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi akipokea salamu ya utii kutoka kwa askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Maafisa wa Mamlaka ya
Hifadhi ya Ngorongoro (hawapo pichani) wakati wa ufungaji mafunzo kwa
askari na maafisa hao yaliyofanyika katika kambi ya mafunzo ya Mlele
mkoani Katavi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii
Meja Jenerali Gaudence Milanzi akikagua gwaride wakati wa kufunga mafunzo kwa askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na
Maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro yaliyofanyika katika kambi
ya mafunzo ya Mlele mkoani Katavi
Askari na Maafisa wa Hifadhi wakipita kwa heshima mbele ya mgeni rasmi kwa mwendo wa pole na haraka wakati wa ufungaji wa mafunzo ya kijeshi
waliyopata katika kambi ya mafunzo ya Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya
kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii
kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu kutoka mfumo wa kiraia.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja
Jenerali Gaudence Milanzi(kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi wakipokea salamu za heshima kwa kupiga
saluti wakati gwaride likipita mbele kwa heshima wakati wa ufungaji wa mafunzo kwa askari wa shirika la
Hifadhi za Taifa,(TANAPA) na Maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya taifa Ngorongoro. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Bendi ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ikipita mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa ufungaji wa mafunzo ya kijeshi kwa askari na maafisa wa Hifadhi ,Mafunzo yaliyofanyika katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.
Askari
na Maafisa wa Hifadhi za Taifa wakionesha umahiri katika matumizi ya silaha wakati
wakionesha kwa vitendo mafunzo ya kijeshi waliyopata katika kambi ya
Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo
chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu.
Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Witness Shoo (kushoto) pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi Mtango Mtahiko wakifuatilia maonesho ya matumizi ya silaha kutoka kwa wahitimu hao.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akisherehesha wakati wa ufungaji wa mafunzo ya kijeshi kwa askari
na Maafisa wa Hifadhi waliyopata katika kambi ya
Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo
chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu.
Ulengaji shabaha...
0 comments:
Post a Comment