ALIYEKUWA rais wa pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kati ya
tarehe 7 Aprili 1972 hadi 30 Januari 1984, Aboud Jumbe Mwinyi amefariki
dunia mchana wa leo nyumbani kwake Kigamboni, jijini Dar es Saalam baada
ya kuugua kwa muda mrefu.
Kifo cha mwanasiasa huyo mkongwe kimethibitishwa na mmoja wa wanafamilia ya marehemu na anataraji kusikwa kesho Kisiwani Zanzibar
Marehemu Jumbe atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa wa kuiongoza
serikali ya mapinduzi ya Zanzibar akichukua nafasi ya aliyekuwa rais wa
nchi hiyo marehemu Abeid Aman Karume aliyefariki mwaka 1972.
Enzi za uhai wake akiwa rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar
alishirikiana na rais wa wakati huo wa Tanzania na mwenyekiti wa chama
cha TANU marehemu Julius Nyerere kuanzisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa
kuvunja vyama vya TANU na ASP na kuunda chama kimoja cha CCM.
Alhaji Jumbe aliwahi kutoa wosia wake hadharani akitaka mazishi yake yasibene sura ya kitaifa na wala jeneza lake lisifunikwe bendera ya taifa au ya chama na kuomba yawe ya mazishi ya Muislamu na mwananchi wa kawaida.
0 comments:
Post a Comment