Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na wadau wa sayansi wakati wa kufungua Kongamano la Tano la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)Dkt. Hassan Mshinda
akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Tano la Kitaifa la
Sayansi, Teknolojia na Ubunifu jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu
wa Tume ya Sayansi Afrika Kusini, Tami Mseleku akizungumza na waaandishi
wa habari jijini Dar es Salaam leo katika ufunguzi wa Kongamano la Tano la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako kulia akiwa katika ufunguzi wa Kongamano la Tano la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifujijini Dar es Salaam leo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Baadhi ya wanasayansi wakiwa katika kongamano la wanasayansi jijini Dar es Salaam leo.
Waziri
wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako
akitembelea maonesho ya wanasayansi mara baada ya kufungua Kongamano la Tano la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifujijini Dar es Salaam leo.
Waziri
wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako akipata
maelekezo juu ya kifaa kinachopiga picha za Juuu(Drone) jijini Dar es
Salaam leo mara baada kufungua Kongamano la Tano la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu
Waziri
wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako akipata
maelekezo katika banda la wanasayansi jijini Dar es Salaam leo mara
baada ya kufungua Kongamano la Tano la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu
*************
Na MICHUZI MEDIA GROUP
TUME
ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imeaswa kuhakikisha tafiti
zinazofanywa zijikite katika kutoa matokeo yatakayoweza kutatua matatizo
ya wananchi na kuendelea kutengeneza ajira ili kuinua kipato cha
wananchi na uchumi wetu kwa ujumla.
Wito
huo umetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof.
Joyce Ndalichako wakati wa kuzindua Kongamano la Tano la Kitaifa la
Sayansi, Teknolojia na Ubunifu jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa
Katika Kutekeleza agizo la Uchumi wa viwanda tunategemea rasilimali watu
yenye ufahamu, ujuzi, teknolojia na ubunifu ili kuzalisha kwa tija na
kuhimili ushindani wa kimataifa.
Profesa
Joyce amesema kuwa Tafiti zilenge katika kuimarisha uchumi wa viwanda
zikiwa ni muhimu katika kuinua tija na uzalishaji, “Baadhi
ya tafiti za Kilimo zilizofanywa na taasisi zetu kama vile Chuo Kikuu
cha Sokoine zimefanikiwa kutoa matokeo mazuri. Hii inajumuisha mbegu
bora zinazoongeza mavuno kama vile mbegu za mihogo, mahindi na mpunga
ambazo zinavumilia ukame na zinaweza kukinzana na magonjwa”. Amesema
Profesa Joyce.
Aidha amewaomba wakamilishe mapema taratibu zinazohitajika ili watanzania wengi waweze kunufaika na chanjo hizo muhimu kwa wafugaji wa kuku.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)Dkt. Hassan Mshinda amesema kuwa tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imeweza kupata chanjo inayozuia magonjwa ya kuku kama vile mdondo, ndui na mafua katika chuo Kikuu cha Sokoine.
0 comments:
Post a Comment