Wakulima wakipalilia mashamba yao ya mizabibu mkoani Dodoma
Mche wa mzabibu shambani kabla ya mavuno
“Kwa muda mrefu
wakulima wa zabibu mkoani Dodoma tumekuwa tukikabiliwa na changamoto mbalimbali
kiasi kwamba licha ya kufanya kazi za kilimo hususani cha mazao ya biashara
tumekuwa tukiendelea kukabiliwa na tatizo la kutopata faida na kubaki katika
hali duni za kutuwezesha kupata mahitaji muhimu ya kukidhi mahitaji yetu
ikiwemo kujenga nyumba bora na kusomesha watoto wetu”Anasema Yarendi Makuya
,mkulima wa zabibu kijiji cha Handala
mkoani Dodoma.
Anasema kuwa katika miaka ya
karibuni kutokana na kuongezeka kwa wawekezaji katika sekta ya viwanda wakulima
wa zabibu wameanza kupata ahueni ya maisha kutokana na wateja wanaowatembelea
vijijini wakihitaji kununua zao la
zabibu wamekuwa wakiongezeka siku hadi siku hali inayotia matumaini kuwa kilimo
cha zao hilo kina fursa ya kuchangia uchumi na kuinua maisha ya wakulima iwapo
watawezeshwa ipasavyo.
Yarendi aliyekuwa akiongea kwa niaba ya wenzake alieleza kuwa hivi
sasa baadhi ya makampuni yaliyowekeza kwenye viwanda yameanza kujenga ukaribu na kushirikiana na
wakulima ili yaweze kupata malighafi kwa ajili ya viwanda vyao na kuhakikisha
uzalishaji wa zao hili unaongezeka.
Moja ya kampuni aliyoitaja
kuwa hivi sasa imejikita katika kilimo
shirikishi na wakulima wa zabibu na ushirikiano huo umeanza kuonyesha mafanikio
ni kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL) maarufu kama Konyagi iliyopo
chini ya TBL Group ambayo hivi sasa inashirikiana na wakulima kwa lengo la
kuwawezesha kuongeza uzalishaji wa
zabibu kupitia mpango wa Go Farming na
wakati wa msimu inanunua zao hilo kwa bei nzuri na malipo kufanyika bila
urasimu kama ilivyokuwa hapo awali walipokuwa wanauza zabibu kupitia vituo vya
Ushirika na walanguzi wa mazao ambao kwa kiasi kikubwa walikuwa
wakiwapunja katika bei ya kuuzia. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
“Katika miaka ya karibuni tangu tuanze kufanya kilimo kwa
kushirikiana na TDL tumeanza kupata mafanikio hasa ya uwezeshwaji katika kilimo
kwa kupatiwa pembejeo,mbegu,madawa ya kuua wadudu,ushauri wa kitaalamu,uhakika
wa soko na kitu kingine tunachokiona kama muujiza ni kampuni kusaidia kusomesha
watoto wa wakulima kupitia mfuko unaojulikana kama Zabibu Kwanza”.Alisema kwa
furaha na kuongeza kuwa mtoto wake anayeitwa Paschal amewezeshwa kusoma hadi
amemaliza kidato cha nne mwaka jana.
Mkulima mwingine Yohana Petro kutoka kijiji cha Mpunguzi alisema
anachofurahia kupitia ushirikiano na kampuni hii ya TDL ni kusaidia watoto wao kwa kuwapatia mahitaji ya elimu “Watoto
wamekuwa wakisaidiwa kulipiwa ada,pia kampuni imekuwa ikitoa misaada ya
vitabu,madaftari,sare za shule na kuwapunguzia makali ya maisha wakulima wengi kwa kuwa hali zetu za maisha
ni ngumu”.Alisema
Hata hivyo alisema pamoja na changamoto nyingi wanazoendelea
kukabiliana nazo kukuza uzalishaji wa zao la zabibu wanajivunia kuona zabibu
wanaozalisha ni bora na inatengeneza Mvinyo wa kiwango cha juu cha kimataifa.
“Mara nyingi tuonapo Mvinyo uliotokana na zabibu tunazolima tunafurahi sana na
kujivunia zao letu japokuwa wengi wetu hatuna uwezo wa kumudu kutumia vinywaji
hivyo kutokana na kutomudu bei zake”.Alisema.
Kwa upande wake Mtafiti wa
Mazao kutoka kituo cha utafiti wa
Kilimo cha Makutupora Viticulture
Training and Research Center (MVTRC)
,Reon Mrosso amesema kuwa kituo
hicho kinaendelea kufanya kazi na wakulima wa zao la zabibu ili kuwezesha
uzalishaji wa zao hilo kuongezeka.
Mrosso amepongeza makampuni
yanayofanya kazi na wakulima kwa kuwawezesha hususani kwa kuwapatia mbegu na pembejeo za kilimo ikiwemo kampuni
ya TDL ambayo inawezesha wakulima wengi
“Changamoto kubwa kwa wakulima wetu ni vipato duni hivyo wakipatikana
wawekezaji wengi kama TDL na kuwezesha wakulima wengi uzalishaji wa zao hili
utaongezeka na maisha ya wakulima kubadilika kuwa bora zaidi”.Alisema.
Alitoa wito kwa wawekezaji wenye nia ya kusaidia kuunga mkono
jitihada za serikali za kukuza sekta ya kilimo wajitokeza kwa kuwa sekta ya
kilimo bado inazo fursa nyingi za kukuza uchumi wa taifa na kuboresha maisha ya
watanzania na kuongeza kuwa kwenye kilimo cha zabibu bado kuna fursa kubwa ya kuchangia
pato la taifa na kukwamua maisha ya wakulima.
Naye Meneja wa ubora wa
Vinywaji vya Mvinyo wa kampuni ya TDL
,Jackob Mwavika amesema katika kilimo cha zabibu mkoani Dodoma nchini bado kuna
fursa kubwa ya kuzalisha zao hili kwa kuwa japo kuna ardhi ya kutosha na hali
ya hewa na ardhi inaofaa kwa kilimo chake
japo uzalishaji bado ni mdogo kukidhi soko lililopo nchini.
Mwavika alisema kampuni TBL Group tayari imeanza mkakati wa
kushirikiana na wakulima na wadau mbalimbali kuendeleza zao ili na tayari
imeanza kutekeleza mpango wa kilimo shirikishi mkoani humo na wakulima wameanza
kuchangamkia fursa hii ambapo hivi kampuni mbali na kuwapatia wakulima
pembejeo,mbegu na ushauri wa kisasa wa kilimo hivi sasa iko mbioni kuingiza
mbegu bora na za aina mbalimbali za zabibu kutoka nchini ya Afrika ya Kusini
ili kuwawezesha wakulima kuzalisha aina zaidi ya moja za zao hili kama ilivo
kwa sasa.
“Ongezeko la matumizi ya mbegu bora ni moja kati ya vitu vinavyohitajika kuwezesha
kufikia uzalishaji na kukua kwa uchumi,kupunguza umaskini na kufikia lengo la
kuwa na mazao ya kutosha na kuwezesha wakulima kupata mapato mazuri ya
kuwawezesha kukidhi mahitaji yao na familia zao za kupanua shughuli zao za
kilimo”.Alisema Mwavika.
Alisema katika kutekeleza suala hili kampuni inaendelea kukamilisha
mchakato wa kupata vibali vya kuingiza mbegu kwa mujibu wa utaratibu unaotakiwa
kufuatwa na ukikamilika katika siku chache zitaletwa mbegu za aina mbalimbali
zitakazowezesha kupatikana zabibu za aina mbalimbali zinatakazotumika
kutengeneza mvinyo na kwa matumizi ya chakula.
Mwavika alisema zaidi ya wakulima
700 wa zao la zabibu mkoani Dodoma wananufaika na mpango wa kilimo shirikishi unaoendeshwa na
kampuni ya TDL kwa kuwawezesha kuongeza uzalishaji katika mashamba yao ya zabibu. “Tumeanza
kutekeleza mpango huu katika vijiji vya Bihawana, Mpunguzi, Mvumi, Hombolo,
Mbabala, Veyula, Makang’wa, Mzakwe na Mbalawala na tunashirikiana na taasisi ya
Makutupora Viticulture Training and Research Center (MVTRC)”,Alisema.
Alisema kuwa Chini ya mpango huo wakulima wanawezeshwa kupatiwa
utaalamu wa kilimo kwa kushirikiana na taasisi ya Makutupora Viticulture
Training and Research Center (MVTRC) ambapo mafanikio ya mpango huo yameanza
kuleta mafanikio kwa wakulima kupatiwa elimu ya kilimo cha kisasa cha zao la
zabibu na kuanza kufanya utekelezaji kwa kutumia ushauri wa wataalamu wa
kilimo.
Katika kuwapatia wakulima motisha wakulima ili wajiunge na waweze kuboresha maisha yao kupitia kilimo
cha zao la zabibu chini ya mpango huu watoto wa wakulima wa zabibu wamekuwa wakisaidiwa kielimu
kupitia mfuko unaojulikana kama Zabibu
na Shule Kwanza.
0 comments:
Post a Comment