Nafasi Ya Matangazo

November 21, 2026

Na Mroki Mroki, BAJP
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma na mlezi wa Umoja wa wanafunzi wanaosoma  Uhusiano wa Umma Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOPRESA) amesema bonanza la michezo la umoja huo ni zaidi ya bonanza kwani washiriki wanapata fursa ya kujifunza kwa vitendo.

Hayo yamesema na Mlezi wa umoja huo na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Dkt. Mary Kayome wakati wa Bonanza la kwanza la UDOPRESA lililofanyika Novemba 21, 2026 katika viwanja vya Carnival chuoni hapo.

“Kwangu mimi hili ni zaidi ya Bonanza kwani ndani yake kuna mafunzo, burudani, kushirikiana na kufahamiana,  hivyo niwaombe tunapokua na matukio kama haya muwe mnashiriki kwani yanasaidia kuonesha vipawa vyenu,” alisema Dkt. Kayome.

Amesema wanafunzi wanapokua katika matukio kama hayo wanapata fursa ya kujifunza kwa vitendo mafunzo ya darasani, hususani kuandika habari za magazeti , kupiga picha na kuzihariri, kuandaa na kusimamia matukio, hivyo matukio hayo yanatumika kujiendeleza kitaaluma. 

“Tunapokua na matukio kama haya, njoo shiriki kwa moyo mwanzo mpaka mwisho sababu utakachokipata ni zaidi ya bonanza,”alisema Dkt. Kafyome. 

Aidha, amsema Bonanza litakalofuata litakua bora zaidi na litashirikisha wadau wa nje na amewataka viongozi kujipanga ili liwe bora zaidi huku akisisitiza kuwa UDOPRESA ni Jukwaa la kujifunza na kupata maarifa mbalimbali. 

Nae Mwalimu wa Masomo ya uandishi wa Habari aliyeshiriki katika bonanza hilo, Samwel Marwa, amesema kupitia bonanza hilo kuna haja ya kushirikisha wadau mbalimbali na kuandaa maonesho ya kitaaluma na kupitia hayo watu watapata fursa ya kujifunza zaidi na kupata fursa za ajira kupitia vipaji vilivyopo. 

Rais wa UDOPRESA Manase amesema licha ya kua na bonanza la kwanza kuandalia na umoja huo lakini limekua la mafanikio makubwa na kuahidi makubwa zaidi katika matamasha mengine yanayofuata. 

UDOPRESA alianzishwa Mei 24, 2025 ikiwa na lengo la kuwaweka pamoja wanafunzi wanaosoma chuoni hapo kwa lengo la kukuza ujuzi na weledi,kuunganisha wanafunzi, utafiti na mafunzo,  na kufanya maandalizi ya ajira. 









Posted by MROKI On Saturday, November 21, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo