Nafasi Ya Matangazo

August 14, 2016



Meya wa Manispaa ya Temeke, jijini Dar es Salaam, Abdallah Chaurembo (kulia) akiwa ameketi na maofisa wa Benki ya DCB pamoja na wanafunzi na walimu wa shule ya Msingi Msufini, wakati wa kupokea msaada wa madawati 100 kutoka Benki ya DCB, kwaajili ya shule hiyo iliyopo Chamanzi. 
Meya wa Manispaa ya Temeke, jijini Dar es Salaam, Abdallah Chaurembo (kulia) akipokea msaada wa madawati 100 kutoka Benki ya DCB, kwaajili ya shule ya Msingi Msufini iliyopo Chamanzi. Kushoto ni Maofisa wa Benki ya DCB wakikabidhi madawati hayo mwishoni mwa wiki.
 Meneja Mkakati na Ubunifu, Samuel Dyamo akiwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Msufini. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

 wanafunzi wa Shule ya Msingi Msufini wakifurahia madawati mapya ya DCB
BENKI ya DCB imetoa msaada wa madawati 300 yenye thamani ya Sh Milioni 39 kwa Halmashauri tatu za Mkoa wa Dar es Salaam.

Msaada huo wa madawati umetolewa na Benki ya DCB ikiwa ni uungwaji mkono wa juhudi za serikali za kuhakikisha inaboresha mazingira ya kujifunzia kwa kuweka madawati kwa shule za msingi na sekondari.

Akikabidhi sehemu ya madawati hayo kwa shule ya Msingi Msufini iliyopo Kata ya Chamanzi Wilaya ya Temeke ambayo imepata madawati 100, Meneja Mkakati na Ubunifu, Samuel Dyamo jana alisema benki hiyo iliamua kutoa msaada wa madawati 300 jijini Dar es Salaam.

Akimwakilisha Mkurugenzi Mtentanji wa DCB Bank, Edmund Mkwawa, Dyamo alisema kuwa bodi ya wakurugenzi ya benki hiyo ilipopata taarifa ya uwapo wa uhaba wa madawati kwa shule za jijini Dar es Salaam iliidhinisha kiasi hicho cha madawati na kati ya hayo 100 ndio yanakabidhiwa hapo Msufini na mengine yatapelekwa Ilala na Kinondoni.

“Benki hii ni ya wananchi wa Dar es Salaam, na wamiliki wa Beki hii ni kutoka Manispaa zote za jiji hili, hivyo tumeamua kuunga mkono jitahada za serikali katika kuhakikisha kuwa hakuna mtoto anaeketi chini,”alisema Dyamo.

Alisema tangu Benki hiyo ianzishwe miaka 14 iliyo[pita tayarui imesha changia kiasi cha sh milioni 179.2 katika huduma mbalimbali za jamii ikiwepo elimu.

Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Chaurembo aliishukuru Benki hiyo kwa msaada huo na kuzitaka taasisi nyingine za fedha kuunga mkono jitihada hizo.

 “Msaada huu unathibitisha dhahiri kuwa Benki ya DCB ni mali ya wananchi na mmeonesha wazi mnavyowajibika katika kusaidia kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha sekta ya elimu,”alisema Chaurembo.

Chaurembo alisema kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017 asilimia 10 ya bajeti hiyo imetengwa kwaajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vya vijana na wanawake na Benki ya DCB imeridhia kutoa mikopo huo kwa riba nafuu.

Mapema Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Msufini,Yassin Mapunda aliishukuru Benki hiyo kwa msaada huo na kusema kuwa bado shule hiyo inakabiliwa na chanagamoto mbalimbalimbali.

 “Shule inawanafunzi 3,672 lakini hatuna choo hata kimoja, na kupelekea wanafunzi wetu kutumia vyoo vya shule jirani kujisaidia,”alisema Mapunda.
Posted by MROKI On Sunday, August 14, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo