Waendesha baiskeli kutoka mikoa
sita ya kanda ya Ziwa wakijiandaa kuchuana wakati wa Mashindano ya mbio za baiskeli ya Acacia Tufankiwe
Pamoja Cycle Challenge 2016 yaliyofanyika mkoani Shinyanga chini ya yakidhaminiwa
na kampuni ya Madini ya Acacia .

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi ,Asa Mwaipopo akizungumza jambo na Mgeni Rasmi ,Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Anastazia Wambura kabla ya kuanza kwa mashindano ya mbio za Baiskeli.
Mwenyekiti wa chama cha mchezo wa Baiskeli Tanzania (CHABATA) Godfrey Mhagama akieleza sheria mbalimbali za mchezo huo kabla ya kuanza rasmi mbio hizo.
Asa Mwaipopo ,Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi ulio chini ya Kampuni ya Acacia ,akizungumza kabla ya kuanza kwa mashindano hayo yanayofanyika kwa mwaka wa tatu katika mji wa Kahama mkoani Shinyanga.Wengine kutoka kulia ni
Meneja Uendelevu wa Mgodi wa kuchimba Dhahabu wa Buzwagi,George Mkanza,Mgeni rasmi katika mashindano hayo Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Anastazia Wambura na katikati ni Katibu wa Baraza la Michezo (BMT) .Said Kiganja.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Anastazia Wambura akivishwa kofia ngumu kabla ya kufungua Mashindano ya Mbio za Baiskeli ya Acacia Tufanikiwe Pamoja Cycle Challange 2016.





Mmoja wa waendesha Baiskeli akipewa maji na mmoja wa makamisaa wa mchezo huo Aman Vicent wakati mashindano hayo yakiendelea.
Meneja wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano kwa Umma wa Kampuni ya Madini ya Acacia,Necta P Foya akishiriki mashindano hayo kwa upande wa wanawake .

Muonekano wa picha ya juu eneo la Phantom eneo ambako mashindano hayo yalianzia na kumalizikia.
Washiriki wa Mashindano ya Mbio za Baiskeli za Acacia Tufanikiwe Pamoja Cycle Challange 2016 wakihitimisha mbio hizo.
Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog aliyeko Kahama,Shinyanga.
0 comments:
Post a Comment