Meneja wa
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
Mkoa wa Lindi, Bi Nour Aziz (kulia) akiwasilisha ahadi ya shirika hilo ya kuchangia milion 50 katika harambee hiyo iliyoongozwa na Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, mwishoni mwa wiki.
Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya
Jamii (NSSF), Mkoa wa Lindi, Bi Nour Aziz akipeana mkono
na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Shirika la Hifadhi ya Taifa ya Jamii NSSF
Makao Makuu ikishirikiana na Ofisi ya Mkoa wa Lindi Imechanga Jumla ya Shilingi
Milioni 50 Kwa Ajili ya Kuchangia Harambee ya Kusaidia Ujenzi wa Shule ya
Sekondari ya Lindi iliyoungua Moto Wiki iliyopita.
Kwa Kutambua Umuhimu wa Elimu kwa
Watoto Shirika Hilo Kupitia Mkurugenzi Mkuu Wake ,Aliewakilishwa na
Meneja wa Mkoa Bi Nour Aziz Limetoa ahadi hiyo kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kasim Majaliwa Alieongoza Harambee Hiyo Ambayo
Ilihudhuriwa na Wadau Mbali mbali Akiwemo Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya
Nne,Mama Salma Kikwete
Katika Harambee Hiyo Jumla ya Shilingi
Milioni 80 Taslimu zilichangwa Huku Ahadi na Vifaa vya Ujenzi zikifikia
Shilingi Milioni 640 Ambapo Katika Ujenzi Mpya Waziri Mkuu Ameagiza Kujengwa
Jengo la Ghorofa litakalokuwa na Ofisi na Madarasa.
Katika Tukio Hilo la Moto,Jumla Ya
Madarasa 9 na viti na Meza zaidi ya 300,Ofisi 4 na Vyoo Matundu 24
Viliteketea na Moto Uliotokana na hitilafu ya Umeme. (Picha na Abdulaziz
Video, Lindi)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimshukuru Mkuu wa Kitengo cha Mafao NSSF, Bw Juma Namuna, baada ya shirika hilo kuahidi kuchangia Milioni 50.
Waziri Mkuu akisalimiana na Mkuu wa Idara ya Uhasibu NSSF mkoa wa Lindi, Jumbe Dona. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Meneja
wa NSSF Mkoa wa Lindi, Bi Nour Aziz akisalimiana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Lindi
wakati wa Harambee.
Baadhi
ya wafanyakazi wa NSSF-Lindi wakisalimiana ba Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Wafanyakazi wa NSSF Lindi wakiwa na nyuso za furaha baada ya kusalimiana na Waziri Mkuu.
Wafanyakazi wa NSSF Lindi wakiwa na nyuso za furaha baada ya kusalimiana na Waziri Mkuu.
Wafanyakazi wa NSSF Lindi wakiongozwa
na Meneja wa Mkoa wakiwa katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Lindi kwa ajili
ya Harambee Hiyo iliyoendeshwa na Waziri Mkuu.
Baadhi ya
wafanyakazi wa NSSF wakiwa katika harambee hiyo.
Mke wa Waziri Mkuu (kushoto) akiwa na Mkuu wa
Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu.
Mama Salma
Kikwete akiwa katika harambee hiyo.
Mke wa Rais mstaafu wa awamu ya nne, Mama Salma
Kikwete akiwasilisha mchango wake katika Harambee hiyo huku Taasisi ya WAMA
ikitoa ahadi ya kuchangia vitabu vya Shule hiyo.
0 comments:
Post a Comment