Waombolezaji wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu tayari kwa safari ya kutoka uwanjani hapo kuelekea Muhimbili kuhifadhiwa
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, (watatu kushoto),
mbunge wa Nsumve Richard Ndasa, (wanne kushoto) nabaadhi ya waaandishi
na wapiga picha, wakilitama jeneza lenye mwikli wa hayati Joseph Senga,
aliyekuwa Mpiga Picha Mkuu wa gazetila Tanzania Daima, wakati
wafanyakazi wa Swissport wakilitoa jeenza hilo kwenye uwanjawa ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Julai 30, 2016
ulipowasili kutoka nchini India.
Marehemu Senga alifariki katikati ya
wiki hii nchini India, alikokwenda kwa matibabu. Taarifaza ndugu wa
marehemu kuhusu taratibu za mazishi zinasema, Mwili wa marehemu
umehifadhiwa kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo Jumapili
asubuhi utapelekwa nyumbani kwake Sinza, kwa ajili ya ibada fupi na
kisha utapelekwa viwanja vya Sinza-Uzuri kwa wananchi ndugu jamaa na
marafiki kuuuaga. Taarifa hiyo pia inasema, Mwili wa Marehemu
utasafirishwa baada ya zoezi la kuuaga Jumapili Julai 31, 2016. (PICHA
NA K0-VIS MEDIA/Khalfan Said)
Ndugu wa karibu akitokwa na machozi baada ya kuona jeneza lililobeba mwili wa marehemu Senga likiwasili
Waombolezaji wakisubiri mwaili kuwasili kutoka nchini India, kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
Othmani Michuzi,(kulia). wa Blog ya Mtaa kwa Mtaa, akimfariji mpiga picha wa Tanzania Daima, Loveness Bernard ambaye alifanya kazi ofisi moja na marehemu Senga
Baadhi ya wapiga picha na waombolezaji wengine wakiondoka baada ya mwili kuwasili
Mbunge wa Nsumve, Richard Ndasa, (kushoto) akimsikiliza, Gabriel Nderumaki wakati wakisubiri mwaili wa marehemu Senga kuwasili
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kulia), akiteta jambona Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima, Neville Meena, wakati wakisubiri kuwasili kwa mwili wa marehemu Joseph Senga, aliyekuwa mpiga picha mkuu wa gazeti hilo
Gari lililobeba jeneza lenye mwili wa marehemu Senga, likiwa tayari kuondoka uwanjani hapo
Msafara wa magari ukiwa tayari kuondoka
0 comments:
Post a Comment