Meneja Masoko na Udhamini wa TBL Group, George Kavishe akizungumza na wanahabari kuhusu kampeni ya Uza, Nunua na ushinde na Konyagi yaliyofanyika jijini Mwanza jana wengine pichani ni maofisa waadamizi wa kampuni hiyo.
Meneja Mauzo wa Konyagi Kanda ya Ziwa, Joseph Mwaigomole akizungumza na wasambazaji wa Konyagi wa kanda hiyo katika mafuzo kuhusu kampeni ya mawakala wa bidhaa za kampuni hiyo ya Uza, Nunua na ushinde na Konyagi yaliyofanyika jijini Mwanza jana.
Wasambazaji wa Konyagi Kanda ya Ziwa wakifuatilia mafunzo ya kampeni ya Uza, Nunua na ushinde na Konyagi yaliyofanyika jijini Mwanza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya mawakala wa konyagi.
TDL yazindua kampeni ya shinda gari kanda ya ziwa
KAMPUNI ya Tanzania Distilleries Limited (DTL) inayotengeneza na kusambaza kinywaji cha konyagi imezindua kampeni ya nunua, uza shinda gari na Konyagi kwa wasambazaji wa bidhaa hiyo .
Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Mwanza juzi, Meneja masoko na Udhamini wa TDL, George Kavishe, alisema kampeni hiyo itashindanisha magari mawili yenye thamani ya Sh milioni 98 na itadumu kwa muda wa miezi mitatu ikilenga kuinua uchumi wa wasambazaji na wauzaji wa bidhaa zao.
Alisema kampeni hiyo itatoa washindi wawili na kwamba watakaopatikana kwa kuzingatia vigezo husika watakabidhiwa magari aina ya Eicher 3 Tonne Truck.
“Mshindi atajishindia gari aina ya Eicher 3 Tonne Truck ambazo zitarahisisha usambazaji wa biashara yake, hivyo kupitia shindano hili tutakuwa tumeboresha usambazaji wa biehaa yetu ya Konyagi, wasambazaji na wauzaji wetu kutoka Kanda nne watashiriki na kila gari ina thamani ya Sh milioni 49.
“Pia kupitia shindano hili kwa kuwa tunaimani mauzo yataongezeka itatusaidia kuweza kushiriki kutatua changamoto mbalimbali za kijamii na kiuchumi kwa wananchi wa hapa nchini,”alisema Kavishe.
Meneja wa Chapa ya Konyagi, Martha Bangu, alisema katika shindano hilo wasambazaji na wauzaji wa bidhaa hiyo wamewekewa viwango ambapo kiwango cha chini ni katoni 400 na cha juu ni 30, 000 na washiriki wote watakaokidhi vigezo wataingia kenye droo kubwa ya kupata mshindi inayotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
Tunaamini kampeni hii itaongeza ufanisi kwa wasambazaji wetu nao wataongeza kiwango cha ununuzi wa bidhaa zetu , shindano hili ambalo limeanza Julai mwaka huu litaisha mwezi Septemba mwaka huu na litajumuisha wasambazaji wetu wote waliopo mikoa ya kanda ya ziwa, Nyanda za juu kusini , Kaskazini, Pwani na Kati,”alisema Bangu
0 comments:
Post a Comment