Nafasi Ya Matangazo

July 21, 2016

Na Mroki Mroki
Julai 5, mwaka huu nikiwa Mkoani Kigoma, nilianza kuposti katika mtandao wangu wa Instagram mtiririko wa hadithi picha niliyoipa jina la Thamani ya Jiwe! Niliamua kupa jina hilo kutokana na namna ambavyop wengi wetu tunayaona mawe kama si kitu chenye thamani sana labda tu kama unahitaji kujengea ambapo utahitaji mawe makubwa kwa kokoto ndogo ili ukamilishe ujenzi wako. 

Lakini ukweli uliopo ni kuwa Jiwe kubwa au dogo linaweza kutumika katika mambo mengi, zamani wazazi wetu waliyatumia kusagia nafaka, na hata wahunzi walichonga nyenzo mbalimbali za kutumia kama majembe, mapnga, visu na mikuki kwa kutumia mawe.

Leo hii katika maeneo mbalimbali ya nchi ambayo yanapatikana mawe mazuri na kama kuna wajenzi wa barabara au majumba utaona kuna mashine za kupasulia kokoto katika maeneo hayo. 

Ndugu zetu wa china wao wamefika mbali mawe yetu hasa pale Msolwa Mkoani Pwani/Morogoro wanayakata kwa ufundi na kutoa vigae vya sakafu na ukutani "tails' ambazo huzisafirisha kwenda kwao na kunakishiwa vizuri na kisha kurejeshwa hapa kwetu vikiwa vimeongezwa thamani kwa kuwekwa kwenye boxi zuri na kuvinunua kwa bei ya juu hii nayo ni THAMANI YA JIWE.
THAMANI YA JIWE! Hapa natumia jiwe hili kuwaeleza ni kwa jinsi gani msanii huyu ameweza kunipa somo mimi binafsi na sasa naamua kuwapa kile ambacho nimekielewa mimi kutokana na JIWE hilo na Msanii huyu.

Jiwe kama jiwe ni sawa na rasilimali nyingi ambazo watanzania katika nchi Yetu nzuri tumejaliwa kuwa navyo, Nchi imejaliwa kwanza watu wazuri na hodari waliona uwezo wa kujibidisha na kujitafutia ridhiki, pia nchi inao watu wabunifu na wasomi wa nyanja mbalimbali na wengi wao kwa sasa ni vijana walio na elimu na nguvu.

Lakini pia nchi yetu Tanzania imejaliwa rasiliamali Ardhi iliyo na Madini, yenye thamani kubwa zaidi duniani japo yapo ardhini. Lakini pia tuna mito, maziwa na mabwawa mengi ambayo yamejaaliwa maji yakutosha. Hizi ni fursa.
Jitihada na bidii binafsi ndicho kitu pekee nadhani tumekikosa pamoja na ubunifu wa kutumia fursa zilizopo kubadili maisha yetu hasa vijana ndicho kitu ambacho tumekikosa licha ya wengi wetu kuwa na elimu ya darasani na ile ya mtaani.
Tuwe wabunifu wakuona kwanza vitu vilivyotuzunguka kama ni moja ya fursa na tunapaswa kuzichangamkia ii zitutoe kimaisha. Hebu tuanze kuongeza thamani ya rasilimali tulizo nazo. Fikiria tu kipande cha ardhi ambacho unaweza kulima kwa kufuata utaalam wa kisasa na kuweza kujipatia mavuno bora na kuweza kupata kipato zaidi ya mwajiriwa.

Kwakutumia kipande kidogo cha ardhi unaweza kufuga, kuku wa kienyeji na hata samaki na kujipatia kipato mara dufu. Tumekosa tu kujiongeza! Kubuni na kufanya kazi kwa bidii kama ambavyo tunaona Msanii huyu Mzungu anavyo chonga jiwe na kuliongeza thamani mara dufu.
JIWE ambalo labda ungeweza kuliuza kwa mponda kokoto kwa sh 10,000 sasa linaweza kuuzwa hata Milioni 5. Sijui wewe msaanii wa uchongaji uliyopo Singida, Iringa, Morogoro, Kigoma na Mwanza au Kagera ambaye unalia hakuna tena miti ya Mpingop ya kuchonga vinyago, ilhali umekalia jiwe ambalo ni imara kuliko Mti wa Mpingo ambao ni nyara ya taifa kwa sasa unajisikiaje.

Yes! Umekalia Jiwe unawaza hakuna miti ya Kuchonga vinyago. Hahahaa Umekalia uchumi, nyanyuka, kuwa mbunifu na sasa kamata fursa hiyo ya Mawe yachonge sanamu kubwa kwa ndogo na utaona faida yake.
Anza sasa kutumia fursa uiyonayo na kipaji ulicho jaaliwa na Mungu kwa kuinua maisha yako. Utaliaje huna hata shiingi ilihali nyumbani kuna eneo unaweza hata kulima mchicha? Mboga mboga zinalipa na wala haziihitaji eneo kubwa. 

Kwanini unapanda maua kuzunguka nyumba na unayamwagilia maji kila siku ilhali unaweza kupanda spinachi katika makopo yako hayo na kuwauzia majitrani na kupata fedha na huku nyumbani kwako pakawa bado panaonekana kwa kijani.

Halafu kijana unatembea na vyeti na kubadili bahasha kila kukicha na kusaka ajira. Huenda hata wazazi wako wanasikitika kujenga jumba kubwa lakini unashindwa kulitumia kwa kupanda mbogamboga.
Vijana ndio taifa a leo hapa Tanzania, tukiweza kujituma kwa bidii hakika matunda tutayaona muda si mrefu. Wasiliana na wenzako ambao mlikutana shule aidha sekondari au Vyuoni na kuwauliza huko wanakotoka kuna fursa gani? Maana leo mimi natoka Kinyenze, Pale Mvomero Mkoani Morogoro, tumejaliwa kuwa na ardhi walau heka tano na wewe mwenzangu umetokea Masaki au Oysterbay jijini Dar es Saaam, Mzazi wako anaweza kukupa Sh 1,000,000/= kama mtaji na ukaja na pampu tu ya maji na pembejeo nyingine hapa Kinyenze na tukalima mboga mboga maana mimi nilikosa mtaji na baada ya mwezi tunafika mbali.

Tufikirie kujiajiri zaidi Tuongeze Thamani ya JIWE letu ambalo ama ni akili zetu au Ardhi na Chochote tulicho nacho na hakika tutaweza kujikwamua. Tusitumie mawasiliano kwa kupeana taarifa tu za C & P.
Tukifanya kazi kwa nidhamu na utuivu kama ambavyo msaanii huyu anaechonga jiwe hili itaweza kutupa faida sana na wengi wakavutiwa na sisi na kutuiga.
Utakapo anza kazi usikate tamaa fanya kazi kwa bidii hata watu wakisema vipi wewe songa mbele na daima mtafutaji hachoki na akichoka kapata.
Tumia kila anina ya nyenzo ulizonazo katika kufikia malengo yako. Amini kuwa elimu au ujuzi uionao unatakiwa tu kutumika na mtu mwingine na kujipatia kisha yeye afikirie namna ya kukulipa. AJIRA NI UTUMWA. Jiajiri kutumia fursa zilizo kuzunguka ili ujikomboe katika Utumwa huo.
Hadithi hii ya JIWE LILILOONGEZWA THAMANI binafsi imenipa somo kubwa sana, nahata wewe naamini imekupa somo, kuwa kumbe inawezekana kutumia kitu fuani kubadilisha na kuwa cha namna ingine na kizuri zaidi.
Kuwa Smart katika maamuzi yako na uyaheshimu maamuzi hayo kwa kuyafanyia kazi. Usikubaliwa kuyumbishwa na vitu ambavyo naweza kuvifananisha na vumbi. Ona Msanii wetu licha ya vumbi la msasa lakini amevaa nguo nyeupe. Jitose kulima au kufuga na kufanya kazi halali bila kujali kiwango cha elimu ulicho nacho kuwa watu watakuonaje.
Binafis nakumbuka miaka ya mwanzoni ya 2000 licha ya kuwa na Diploma yangu ya Uandishi wa habari lakini nilikuwa nimejibidisha sana katika kilimo nikiwa pale Kibaha. Nikilima Mahindi chini ya Nguzo za Umeme za Gridi ya Taifa, nililima zaidi ya Heka mbili na nilihudumia vizuri shamba lile na kila aliyepita alitamani liwe lake. 

Sikuwa na muda wa kukaa vijiweni labda usiku kuanzia saa moja huko ili nijue tu kunanini duniani. Nakumbuka Mwalimu mmoja aliyekuwa akifundisha Chuo fani maeneo yale akikaa Mwanalugali aliniita asubuhi moja na kuniuliza vitu kutokana na jinsi ninavyo jituma akaniambia anatamani vijana wake nao wawe kama mimi maana wakwake wamemaliza kidato cha nne tu lakini wanajiona wasomi hawayaki kujituma kufanya chochote akini mimi na Diploma yangu nilisha jembe.
Hivyo usidhani kama elimu uliyonayo na ujuzi ulio nao kama utautumia kwa kutembea na vyeti tu mkononi vitaleta tija. Bali tuamke sasa na kutumia fursa zinazotuzunguka. Inawezekana sijasema kia kitu lakini nimegusia tu namna gani unaweza kutumia fursa uiyonayo kwa vitu ulivyonayo katika mazingira yetu tunayoishi. Usibaki kama Jiwe.  Ambalo lenyewe haliwezi kujibadili hadi libadilishwe, sasa wewe usingoje kuwa jiwe kwa kubadiishwa na kuwa kitu fulani.
Jiwe Lililoongezwa Thaani...
Posted by MROKI On Thursday, July 21, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo