Meneja usalama ,afya na mazingira wa TBL Group Renatus Nyanda,akitoa
mafunzo kwa wanachama wa Chama cha waajiri Tanzania( ATE) wakati walipokwenda
kujifunza mambo mbalimbali yanayohusiana na usalama sehemu za kazi kwenye
kiwanda cha TBL Ilala jijini Dar es Salaam.
Wanachama wa Chama Cha Waajiri Tanzania(ATE) wakimsikiliza kwa makini
mtaalam wa upishi wa TBL Group Castor Masawe, kuhusiana na uzalishaji
wa bia unavyofanyika.
Kutokana na kampuni ya TBL Group kuonyesha mafanikio ya kuwa
mwekezaji bora nchini na mchango wake kutambuliwa na taasisi mbalimbali kwa
kuitunukia tuzo ,imekuwa kivutio kikubwa kwa taasisi zinazotaka kupata
mafanikio kwa kutembelea viwanda vyake kwa ajili ya kupata mafunzo na
uzoefu na kujua siri ya mafanikio.
Wanachama wa Chama cha Waajiri nchini (ATE) wamefanya ziara katika
kiwanda cha TBL cha Ilala ambako wamepatiwa mafunzo ya usalama kazini ikiwemo
kuona uzalishaji unavyofanyika kiwandani hapo. BOFYA HAPAKUSOMA ZAIDI
Meneja Usalama,Afya na Mazingira wa TBL Group,Renatus Nyanda aliwapatia
somo la kanuni za usalama zinazotekelezwa na kampuni hiyo ambazo zinalenga
kulinda usalama wa wafanyakazi wanapokuwa kazini na nje ya kazi ikiwemo wageni
mbalimbali wanaofika kiwandani hapo.
Wanachama hao walifurahishwa na mafunzo hao ikiwemo mkakati wa
kampuni hiyo kuendelea kufanya uwekezaji unaozingatia utunzaji wa
mazingira,kuchangia kuendeleza uchumi wa taifa,kupunguza tatizo la ajira na
kubadilisha maisha ya jamii kuwa bora.
Meneja usalama ,afya na mazingira wa TBL Group Renatus Nyanda,akitoa
mafunzo kwa wanachama wa Chama cha waajiri Tanzania( ATE) wakati walipokwenda
kujifunza mambo mbalimbali yanayohusiana na usalama sehemu za kazi kwenye
kiwanda cha TBL Ilala jijini Dar es Salaam.
Wanachama
wa Chama cha Waajiri (ATE) wakipewa maelekezo na Meneja usalama ,afya na
mazingira wa TBL Group Renatus Nyanda wakati walipotembelea chumba cha maabara
cha TBL Ilala jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wanachama cha Waajiri Nchini (ATE) wakiangalia vikombe vya
tuzo mbalimbali ambavyo TBL Group ilishinda
0 comments:
Post a Comment