Naibu
Waziri wa Habari, Uramaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia James Wambura (wane kushoto),
akipeana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Ting, Father Fernandez,
wakati akipokea msaada wa mageti kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
Juni 17, 2016. Kampuni hiyoimetoa mageti 27 yenye thamani ya shilingi milioni
44.
Mkurugenzi
wa kampuni ya Ting, Mchungaji Dkt. Vernon Fernados, akimuonyesha moja
ya mageti hayo Naibu Waziri Anastazia James Wambura
Naibu
Waziri akizungumza wakati wa makabidhiano hayo. Kushoto ni Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Michezo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Alex Nkenyenge. BOFYA HAPAKWA TAARIFA ZAIDI
NA
K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID
KAMPUNI
YA kusambaza ving'amuzi vya televisheni ya Ting ya jijini Darves Salaam,
imekabidhi mageti ya chuma 27 kwa
uongozi wa uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam ili kuwadhibiti “wakora” wanaoingia
kwenye vyoo na kuiba koki za maji.
Akipokea
msaada huo leo Juni 17, 2016 kwenye hafla fupi iliyofanyika uwanjanin hapo,
Naibu Waziri wa Habri, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia James Wambura, ameishukuru
kampuni hiyo kwa msaada huo ambao utakomesha vitendo vya wizi na uharibifu wa
miundo mbinu ya uwanja huo wa soka wa kisasa kabisa hapa nchini
“Mwanzoni
mwa mwezi wa tatu mwaka huu, nilifanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya
uwanja huu na kujionea uharibifu mkubwa kwenye vyoo ambapo koki za maji
zimeibiwa na hivyo kusababisha baadhi ya vyoo kufungwa na kupelekea usumbufu
mkubwa kwa mashambiki was ok.” Alisema Naibu waziri.
Naye
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Ting, Mchungungaji Dkt. Veron Fernandos, alisema kampuni yake
ambayo inajishughulisha na uagizaji na usambazaji wa ving’amuzi, imeona inao
wajibu mkubwa wa kusaidia sekta ya michezo kwenye eneo hilo la kutunza
miundombinu ya uwanja wa Taifa.
Alisema,
Ting imetoa jumla ya mageti 27 yenye thamani ya shilingi milioni 44 ambayo
yatasaidia kudhibiti wezi wanaoingia kwenye vyoo na kuiba koki na kuharibu
miundombinu mingine.
K-VIS
MEDIA imeshuhudia koki za maji kwenye baadhi ya vyoo zikiwa zimeng’olewa.
Mkazi wa jijini Dar es Salaam, akitoka kwenye vyoo vya juu vya uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambavyo vimeathirika sana na wizi huo, Mageti hayo yatafungwa kwenye vyoo hivyo vya juu uwanja mzima
Mkazi wa jiji akijisaidia kwenye moja ya vyoo hivo huku upande wa kushoto bomba linaonekana likiwa limeng'olewa koki
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Michezo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Alex Nkenyenge, (kushoto), akizungumza mbele ya Naibu Waziri, Wambura (katikati) na Mkurugenzi wa Ting, Dkt. Fernados
Naibu Waziri akizungumza na Kaimu Meneja wa Uwanja wa Taifa, Julius Mgaya, wakati akiwasili kwenye hafla hiyo
Kaimu Meneja wa Uwanja wa Taifa, Julius Mgaya, (katikati) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Ting, Dkt. Fernandos, wakimpokea Naibu Waziri
Naibu Waziri akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ting, Dkt. Fernandos, wakati akiwasili uwanja wa Taifa kupokea mageti hayo
Sehemu ya uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambao baadhi ya watu wamekuwa wakihujumu miundombinu yake
Wafanyakazi wa kampuni ya Ting
Mkurugenzi Mtendajiw a Kampuni ya Ting, akiwa na baadhi wa wafanyakazi na wawakilishi wa kampuni hiyo kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara
Nyasi za uwanja wa Taifa zikipunguzwa kwa mashine maalum
0 comments:
Post a Comment