Wafanyakazi wa kampuni ya TBL Group wakishiriki kusafisha mazingira ya eneo la Ilala kota jijini Dar es Salaam,jana katika kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani
Wafanyakazi wa kampuni ya TBL Group wakishiriki kusafisha mazingira ya eneo la Ilala kota jijini Dar es Salaam,jana katika kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani
Wafanyakazi wa kampuni ya TBL Group wakikabidhi baadhi ya vifaa vya kufanyia usafi kwa viongozi wa serikali ya mtaa wa eneo la Ilala jijini Dar es Salaam
KAMPUNI ya TBL Group wameshiriki kuadhimisha siku ya
Mazingira Duniani kwa vitendo ambapo wameshiriki katika zoezi la kusafisha
mazingira katika eneo la Ilala Kota kwa kushirikiana na
wafanyakazi wa manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam ambapo pia
kampuni imetoa msaada wa vifaa vya kufanyia usafi vyenye thamani ya
shilingi milioni 6 kwenye kata hiyo.
wafanyakazi wa viwanda vingine vilivyopo
chini ya kampuni pia wameshiriki katika zoezi la kufanya usafi katika maeneo ya
viwanda vyao na maeneo ya jirani kwa
kushirikiana na wananchi wanaoishi kwenye maeneo hayo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Akiongea juu ya maadhimisho hayo Meneja wa
kiwanda cha TBL cha Ilala,Calvin
Martin amesema kuwa wafanyakazi wa kampuni
ya TBL Group popote walipo
wameshiriki kuadhimisha siku hii kwa kuwa mazingira ni
moja ya mtazamo wa kampuni ambapo
imelenga kufanya uzalishaji usio na athari kwa mazingira.
“ Moja ya malengo ya kampuni ni
kujenga dunia imara na dunia iliyo
safi ambayo yamelenga kupata raslimali ya pamoja ya maji ya kutosha ambayo
inatumika kwa kiasi kikubwa katika biashara ya kampuni.Katika kutekelea lengo
hili kampuni kwa muda mrefu imekuwa mstari wa mbele kulinda na kutunza
vyanzo vya maji na kuhakikisha maji yanayopatikana yananufaisha jamii ya
wananchi inayowazunguka”alisema Calvin.
Calvin aliongeza kusema kauli mbiu ya siku
ya mazingira duniani mwaka huu isemao “Tuhifadhi vyanzo vya
maji kwa uhai wa taifa letu”.inakwenda sambamba na malengo ya kampuni ya TBL Group
ambayo pia ina mkakati wa kuelimisha jamii kutunza vyanzo vya maji na kusaidia
kuendeleza miradi ya maji nchini.
Alisema katika kutekeleza utunzaji wa
mazingira kwa vitendo TBL Group imeanza kufanya uzalishaji wa kutumia pumba za mpunga katika
kiwanda chake cha Mwanza na inafanya mkakati kuhakikisha inafanya uzalishaji
usio na athari kwa mazingira katika viwanda vyake vyote,
“Kampuni mama ya SABMiller imejiwekea
malengo hadi kufikia mwaka 2020 kuhakikisha inafanya uzalishaji kwenye viwanda
vyake usio na athari za mazingira hususani uchafuzi wa hali ya hewa au kufanya
uharibifu wa mazingira wenye athari kwa jamii zinazoishi karibu na maeneo
vilipo viwanda vyake kwa asilimia 50% na tayari hadi kufikia sasa imepunguza
uchafuzi wa hali ya hewa unaotokana na uzalishaji kwa asilimia 35% tangia
kuanza kwa mkakati huu mnamo mwaka 2008”.Alisema.
0 comments:
Post a Comment