Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
(kulia) akizungumza na Rais wa Comoro Mhe.Azali Assouman walipokutana kwenye
uwanja wa ndege wa Dar es Salaam ambapo Rais huyo wa Comoro alikuwa kwenye
mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na safari ya kwenda Macca kwenye ibada ya
Umrah nchini Saudi Arabia.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa
tatu kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Comoro
Mhe.Azali Assouman na ujumbe wake walipokutana kwenye uwanja wa ndege wa Dar es
Salaam ambapo Rais huyo wa Comoro alikuwa kwenye mapumziko mafupi kabla ya
kuendelea na safari ya kwenda Macca kwenye ibada ya Umrah nchini Saudi Arabia.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza
na Balozi wa Japan nchini Mhe. Yoshida Masaharu Ikulu jijini Dar es Salaam
ambapo Balozi wa Japan Nchini alisema nchi yake imeridhishwa na kasi ya
Serikali ya Rais Mhe. Magufuli na kuahidi kuendelea kuisaidia Tanzania
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa
kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Japan nchini Mhe. Yoshida Masaharu mara
baada ya mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.
*********************
Rais wa Comoro AzaliI Assouman amesema serikali yake itaendelea
kudumisha uhusiano na ushirikiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Comoro
katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu,afya na biashara.
Rais huyo wa Comoro ametoa kauli hiyo katika uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya
mazungumzo na Makamu wa Rais wa
jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais John Pombe Magufuli
akiwa kwenye mapumziko mafupi kabla ya kuendelea
na safari yake ya Mecca – Saudi Arabia kwa ajili ya ibada ya UMRAH.
Rais Azali Assouman pia amepongeza jitihada zinazofanywa na serikali ya
awamu ya Tano zinazolenga kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata huduma bora
za kijamii na kusisitiza kuwa serikali yake itaendelea kujifunza kutoka
Tanzania ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Komoro.
Akitoa ujumbe wa Rais JOHN MAGUFULI kwa Rais wa Comoro Azali assouman, Makamu wa Rais
Samia Suluhu Hassan amemhakikishia Rais wa Comoro kuwa Tanzania itadumisha
uhusiano uliopo kati ya nchi hizo MBILI hasa kwenye sekta za elimu, afya na
biashara kwa ajili ya manufaa ya nchi hizo MBILI.
Makamu wa Rais pia amemtakia Rais wa Comoro kheri katika safari
yake ya Mecca– Saudi Arabia kwa ajili ya Ibada ya Umrah.
Wakati huo huo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia
Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa JAPAN hapa nchini
Masaharu Yoshida na kumweleza kuwa serikali itaendelea kuweka na kuboresha
mazingira bora kwa ajili ya wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali Duniani
ikiwemo wawekezaji kutoka nchini JAPAN.
Makamu wa Rais amesema serikali ya JAPAN imekuwa mshirika mkubwa wa
maendeleo kwa Tanzania katika kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo Tanzania
Bara na Visiwa hasa kwenye sekta ya elimu, afya na maji na kusema jambo hilo ni
zuri na lakuigwa na washirika wengine wa maendeleo.
Kwa upande wake Balozi wa Japan hapa nchini MASAHARU YOSHINDA
amemhakikishia Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN kuwa nchi yake itaendelea
kufadhili ipasavyo miradi
ya maendeleo hapa nchini ili kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata huduma
bora za kijamii.
0 comments:
Post a Comment