Waziri wa Habari, Utamanduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akipinga mpira kuashiria uzinduzi wa rasmi wa michuano ya Airtel Rising Stars 2016. Uzinduzi huo umefanyika Jumapili 26 Juni 2016 kwenye makao makuu ya Airtel Tanzania Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano akimuonesha Waziri wa Habari, Utamanduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys waliopatiakana kupitia michuano ya Airtel Rising Stars wakati wa uzinduzi wa awamu ya sita ya michuano hiyo uliofanyika Dar es Salaam Jumapili Juni 26 2016.
Waziri wa Habari, Utamanduni ,Sanaa na Michezo Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa michuano ya Airtel Rising Stars 2016 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano akiongea wakati wa uzinduzi wa msimu wa 6 wa Airtel Rising Stars
Rais wa TFF Jamal Malinzi akiongea wakati wa uzinduzi wa msimu wa 6 wa Airtel Rising Stars
Waziri wa Habari, Utamanduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye (katikat) akiwa katika picha ya pamoja na viongezi wa TFF pamoja na Airtel Mara baada ya uzinduzi wa Msimu wa sita wa michuano ya Airtel Rising Stars
Wafanyakazi wa Airtel wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari, Utamanduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye wakati wa uzinduzi wa wa Msimu wa sita wa michuano ya Airtel Rising Stars. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
******************
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Nape Nnauye
leo amezindua msimu wa sita wa mashindano ya soka ya vijana chini ya umri wa
miaka 17 ya Airtel Rising Stars na kuwapongeza Airtel Tanzania kwa kuendelea
kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali pamoja na shirikisho la mpira wa
miguu nchini (TFF) za kukuza mchezo wa soka.
“Programu za soka za vijana ndiyo muhimili wa maendeleo ya soka popote
pale duniani. Ndiyo maana nasisitiza umuhimu wa mashindano ya Airtel Rising
Stars ambayo matunda yake yameonekana dhahiri katika kipindi cha miaka mitano
iliyopita”, alisema Nnauye.
Alitoa mfano wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17
Serengeti Boys ambayo wachezaji wake 10 wa kutumainiwa wametokana na Airtel
Rising Stars. “Matunda ya Airtel Rising Stars vilevile yanaoneka dhahiri kwenye
timu ya taifa ya wanawake Twiga Stars ambayo wachezaji wake wote wanatokana na
programu hii ya vijana”, alisema Nnauye. Klabu za daraja la kwanza na ligi kuu
Tanzania bara pia zinafaidi matunda ya Airtel Risings Stars.
Waziri amewataka viongozi wa soka kusimamia vizuri pragarmu ya Airtel
Rising Stars ili kuweza kubaini vipaji vingi zaidi kupitia mashindano haya ya
vijana ya kila mwaka yakishirikisha timu za wasichana na wavulana kuanzia ngazi
ya mkoa na kuhitimishwa kwa fainali ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa
Airtel Tanzania Beatrice Singano alimhakikishia waziri kuwa kampuni ya Airtel
Tanzania ina nia thabiti ya kuendelea kudhamini michuano hiyo ambayo imesaidia
kuzalisha wachezaji wengi chipukizi hivyo kuendeleza mchezo huo marufu hapa
nchini.
Alisema Airtel Rising Stars mwaka inafanyika chini ya mwanvuli wa
kampeni ya Airtel RURSA iliyozinduliwa mwaka jana kwa lengo la kuwahamasisha
vijana kutumia fursa mbalimbali walizonazo ili kujiendeleza kiuchumi. “Airtel
Rising Stars yenyewe ni Airtel FURSA kwa kuwa inawawezesha vijana kutumia
vipaji vyao kujikwamua kimaisha kupitia mpira. Mpira ni chano cha kipato cha
kuaminika”, alisema.
“Kwa kuwa na wateja wengi nchi nzima Tanzania bara na Zanzibar, Airtel
Tanzania tunawiwa kuendelea kutoa sehemu ya faida yetu kwa jamii kupitia mchezo
wa mpira wa miguu ambao ni marufu kuliko michezo yote hapa Tanzania. Ni njia ya
kuwashukuru wateja wetu kwa kuedelea kutuunga mkono”, alisema.
Kwa upande wake, Rais wa TFF Jamal Malinzi alisema programu ya Airtel
Rising Stars imeleta mapinduzi na kubadilsha kabisa sura ya mchezo wa soka hapa
nchini. “Nawapongeza Airtel Tanzania kwa kuendelea kutuunga mkono. Naamini
kwamba tutapata mafanikio makubwa zaidi siku za usoni”, alisema.
Airtel Rising Stars mwaka huu itashirkisha timu kutoka mikoa ya Mwanza,
Morogoro, Mbeya, Temeke, Ilala, Morogoro (wavulana) wakati mikoa
itakayoshirikisha timu za wasichana ni Ilala, Kinondoni, Temeke, Arusha,
Lindi na Zanzibar
0 comments:
Post a Comment