Kaimu Katibu
Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri akizungumza wakati wa kufunga
mkutano wa Wachumi na Maafisa Mipango uliofanyika katika ukumbi wa Hazina,
Dodoma.
Kaimu Katibu
Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri akizungumza wakati wa kufunga
mkutano wa Wachumi na Maafisa Mipango uliofanyika katika ukumbi wa Hazina,
Dodoma.
Baadhi ya
washiriki wa mkutano wa Wachumi na Maafisa Mipango wakimsikiliza Kaimu Katibu
Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (hayumo pichani wakati wa
kufunga mkutano wa Wachumi na Maafisa Mipango mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya
washiriki wa mkutano wa Wachumi na Maafisa Mipango wakimsikiliza Kaimu Katibu
Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (hayumo pichani wakati wa
kufunga mkutano wa Wachumi na Maafisa Mipango mwishoni mwa wiki.
*************
Stori
na Picha na Joyce Mkinga
SEKTA Binafsi katika ngazi zote ni lazima ishirikishwa katika
utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo 2016/17 – 2020/21 uliozinduliwa
hivi karibuni.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bibi Florence Mwanri aliyasema
hayo alipokuwa akifunga mkutano wa Wachumi na Maafisa Mipango uliofanyika mjini
Dodoma mwishoni mwa wiki.
Bibi Florence Mwanri amesema sekta binafsi ni wadau muhimu katika
utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo hivyo, wanatakiwa kushirikishwa
katika mipango yote ya Serikali. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
“Katika mipango yetu katika ngazi zote lazima sekta binafsi
ishirikishwe kwa sababu wao ndio watekelezaji wakubwa wa mpango huo” alisema
Bibi Mwanri
Amesema maafisa mipango wanapoibu miradi mbalimbali katika ngazi ya
kijiji, wilaya, mkoa ni lazima sekta binafsi ishirikishwe ili kuwapa fursa
nzuri ya kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa
Maendeleo ambao unalenga katika Kujenga Uchumi wa Viwanda ili Kuchochea Mageuzi
ya Kiuchumi na Maendeleo ya watu
Mkutano huo uliwashirikisha wachumi na maafisa mipango 170 kutoka
katika wizara, idara za serikali, sekretarieti na mikoa na wilaya, taasisi za
utafiti, na sekta binafsi ulikuwa na kaulimbiu ya Kuelekea kwenye Utekelezaji
wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo 2016/17 – 2020/21.
Lengo kuu la Mkutano huo ilikuwa ni kujenga uelewa wa pamoja juu ya
Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano na utelekezaji wake.
Mpango huo unatarajia kugharimu Trilioni 107 ambapo Sekta binafsi
itachangia Trilioni 48.
Akiwasilisha maazimio ya mkutano huo Kaimu Naibu Katibu Mtendaji wa
Tume ya Mipango kutoka Klasta ya Uchumi Jumla, Dkt. Lorah Madete amesema Serikali
na sekta binafsi wakutane pamoja na kupanga mikakati ya kutekeleza mpango huo
wa maendeleo.
Vile vile, Dkt Madete alisema kuwa kuna haja ya Serikali kuingiza
Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia katika mipango ya Serikali ikiwa ni
pamoja na Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano.
Mkutano huo uliandaliawa Tume ya Mipango kwa ushirikiano na Taasisi ya
Uongozi.
0 comments:
Post a Comment