Mkurugenzi wa rasilimali watu wa Airtel, bwana Patrick Foya
akiitambulisha kwa blogger VSOMO mfumo mpya unaomwezesha kijana wa kitanzania
,kupakua masomo ya ufundi stadi yanayotolewa na VETA kupitia simu yake ya
Airtel.
Mlimiliki wa 80/20 blog Shamimu Mwasha akiuliza swali mara baada ya
kupata ufafanuzi juu ya mpango wa VSOMO ushirikiano kati Airtel na VETA kwenye
mkutano ulifatiwa na Futari
Baadhi ya Bloggers wakijaribu kupakua masomo ya ufundi stadi
yanayotolewa na VETA kupitia simu zao na ipad zao. Kushoto ni Jackson Mbando wa Airtel akiwapa maelekezo
wafanyakazi wa Airtel wakipata futari
Mzee John kitime (katikati) wakijadili jambo pamoja na shamimu mmiliki
wa blog ya 80/20 na Josephat Lukaza mmlimiki wa lukaza blog, wakati
wa mkutano wa kuitambulisha VSOMO mfumo mpya unaomwezesha kijana wa kitanzania
,kupakua masomo ya ufundi stadi yanayotolewa na VETA kupitia simu yake ya
Airtel.
Bloggers wakiwekewa uji na chai katika vikombe kutoka kushoto ni Othman Michuzi wa Blog ya Mtaa kwa Mtaa, Ahmad Michuzi wa Blog ya JIACHIE na Mroki Mroki wa Father Kidevu Blog
Father Kidevu akifurahia utamu wa tende
Baadhi ya bloggers wakipata futari
****************
KATIKA mpango wake wa kukutana na kuendelea na mfungo wa mwezi
Ramadhani leo Airtel kupitia Airtel FURSA imekutana bloggers na kuzungumzia
mambo mbalimbali ikiwemo VSOMO mfumo mpya unaomwezesha kijana wa kitanzania
,kupakua masomo ya ufundi stadi na kupata cheti kupitia simu yake ya Airtel.
Akielezea VSOMO Mkurugenzi wa rasilimali watu bwana Patrick Foya
alisema, ana anamatumaini kuwa VSOMO masomo ya Ufundi yanayotolewa na VETA
kupitia simu za mkononi za Airtel, yatakua suluhisho kwa vijana wengi wenye
ujuzi na ari ya kujifunza kufanya shughuli kwa uhakika kwani watakua
wamejifunza mbinu zitakazowawezesha kuto bahatisha na kuongeza ufanisi katika
kazi zao.
Nao bloggers walio hudhuria walikua na haya ya kusema, mfumo huu
utaleta tija sana kwa vijana wengi ambao wako katika shughuli mbalimbali kupata
muda wa kujifunza na kupata taaluma zitakazowawezesha kujiajiri, tunawapongeza
Airtel kwa kuanzia mfumo huu wa masomo kupitia simu.
Aidha waliongeza kwa
kusema wao watakuwa mstari wa mbele kushirikiana na Airtel kwa kuwafikia
makundi mbalimbali ya vijana katika maeneo yao ya kazi ili kuhakikisha
wanaitumia vyema fursa hii katika kujiendeleza kitaaluma.
0 comments:
Post a Comment