Mkurugenzi wa Bodi inayosimamia michezo ya Kubahatisha nchini,Bw, Abbas Tarimba akiwa na Mwenyekiti wa Gidani Group ,Profesa Bongani Aug Khumalo.
Mwenyekiti wa Gidani Group na Makamu wa Rais wa
Shirikisho la Michezo ya kubahatisha katika kanda ya Afrika ya Kusini Profesa
Bongani Aug Khumalo akielezea jinsi
michezo ya Bahati Nasibu itakavyoendeshwa kwa wananchi waliofika kwenye Banda la
Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ambapo kampuni hiyo ilishiriki.
************
MCHEZO mkubwa wa kubahatisha nchini wa Bahati
Nasibu ya Taifa utaanza kuchezwa nchini mwezi huu na tiketi za kushiriki
zitaanza kuuzwa katika mikoa yote
kuanzia Mei 21 mwezi huu ambapo droo ya kwanza itafanyika Mei 28 ambapo mshindi
wa zawadi kubwa atakuwa milionea kwa kijishindia kitita cha shilingi milioni 100.
Mchezo huu kwa sasa utaendeshwa na kampuni ya
kimataifa ya michezo ya Bahati Nasibu ya Gidani International ambayo kupitia
kampuni yake tanzu ya Murhandizwa Limited mwaka jana ilipata leseni ya
kuendesha michezo ya bahati nasibu ya Taifa nchini na kwa muda wote imekuwa
ikijenga mazingira ya kuendesha michezo hii kisasa kutokana na uzoefu wake
mkubwa wa kuiendesha katika nchi mbalimbali. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA.
Bahati Nasibu ya Taifa itachezesha michezo mikubwa
itakayowezesha washiriki kushinda
zawadi kubwa katika mwaka wake wa kwanza wa kuendesha shughuli zake hapa nchini
sambamba na kuweka rekodi barani Afrika na sehemu nyinginezo duniani.
“Katika kusherehekea kuanza kwa bahati nasibu hii
hapa nchini katika michezo ya 6 ya mwanzoni itazalisha mamilionea kwa kuwa
washindi wa droo kubwa watanyakua zaidi ya milioni 1000.Tunategemea maisha ya
watu wengi yatabadilika kuwa bora kupitia bahati nasibu huu pia usambazaji wa
tiketi utafanyika kwa utaalamu mkubwa”.Alisema Profesa Bongani Aug Khumalo, Mwenyekiti wa Gidani
Group na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Michezo ya kubahatisha katika kanda ya
Afrika ya Kusini.
Tiketi za
kushiriki bahati nasibu hii itauzwa shilingi 500 kila moja na zitapatikana nchi
nzima kupitia mtandao wa mawakala wa kampuni pia zitauzwa kwa njia ya mtandao.Maelezo
zaidi ya kushiriki yatatolewa kupitia vyombo vya habari wakati wa kuuza tiketi
ukifika.
Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya
www.nationallottery .co.tz kuanzia Mei 9,pia
taarifa na matangazo juu ya mchezo huu yatapatikana kwenye vyombo vya
habari.
0 comments:
Post a Comment